Binti Leah Mathias mtoto wa Mwandishi Mathias akiwa ameshiriki katika hafla hiyo
Mke wa Mwandishi Mathias Canal Bi Zakati Chagamba akifurahi na Mwanae Leah Mathias wakati wa hafla hiyo, Pembeni ni Teddy Fransis Mpwa wa Mathias Canal
Maelekezo ni muhimu ili kuwa na nidhamu katika kula
Watoto wakifurahia chakula cha jioni pasina vurugu na kadhia yoyote
Mlo unaendelea mpaka kushiba atakaye na aje
Moja wa binti aliyetelekezwa akiwa na watoto wake kushiriki mlo wa chakula cha jioni ulioandaliwa na Mwandishi Mathias Canal
Picha ya pamoja mara baada ya kushiriki Hafla ya chakula cha jioni
Wengine ni wakubwa kabisa lakini wapo mitaani walikuwa watoto wadogo na sasa wamekua watu wazima
Na Mwandishi Wetu, Mwanza
Mwandishi wa
habari na mchambuzi wa masuala ya siasa nchini Tanzania Ndg Mathias Canal tarehe nne ya kila Mwezi wa kumi na mbili
huadhimisha kumbukizi ya kuzaliwa kwake ambapo hii leo ameadhimisha kumbukizi
hiyo kwa kula chakula cha jioni na familia yake sambamba na watoto wa Mitaani
(Street Children) wa JIjini Mwanza waliojitokeza kwenye hafla hiyo ya chakula
cha jioni.
Canal
ameamua kufanya hivyo kutokana na watoto wa mitaani hujitokeza kwa wingi kuomba
msaada wa kupatiwa hela ili wanunue chakula katika eneo maarufu Jijini Mwanza
la Salma Cone ndipo mwandishi huyo
kwa kushirikiana na Asasi isiyokuwa ya kiserikali ya METDO Tanzania walipoamua
kushiriki chakula cha jioni kwa kula na watoto hao.
Akizungumzia
maamuzi hayo ya kukacha kwenda Beach ama maeneo ya kuvinjari kama ambavyo
waadhimishaji wengine hufanya Mathias Canal alisema kuwa ni jambo la thawabu
sana kwa Mungu na kwenye jamii kwa ujumla kushiriki chakula cha jioni na
watotot wa mitaani kwani asilimia kubwa wapo katika mazingira ya kuomba
kutokana na hali ngumu za maisha zinazozikabili familia zao, lakini pia wapo watoto
wengine ambao walitelekezwa na wazazi wao jambo ambalo limesababisha kuwa
katika maeneo yasiyo rasmi na kujihusisha na tabia ovu.
”Serikali
inapaswa kuwa na mkakati mathubuti wa kuwasaidia watoto hawa kwani kuwaacha
waendelee kuwa mitaani ni njia mojawapo ya kuzalisha Wezi na Majambazi, Malaya
na Mashoga hii ni kutokana na vitendo ovu wanavyofanyiana wenyewe kwa wenyewe
watoto hawa au kufanyiwa na watu wengine kwa kubakwa na kulawitiwa” Alisema
Canal
Serikali
kupitia wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto inapaswa kulitaza jambo hili kwa umakini
kwani Tanzania inaendelea kuwa na watoto wengi wa mitaani hususani
katika majiji na maeneo ya mikoa mbalimbali ili kunusuru Taifa lenye vijana
wengi wa badae wasiokuwa na elimu na hatari kwa wananchi wengine kuna kila
sababu ya kuweka mikakati ya kukabiliana na kadhia hiyo.
Kuna taarifa kuwa idadi ya watoto wanaoishi katika mazingira
hatarishi nchini imezidi kuongezeka kwa kasi ya kutisha. Hii inatokana na idadi
hiyo kufikia watoto 897,913, ambao wote wamekuwa wakikabiliwa na hali ngumu ya
maisha inayoambatana na vitendo vya ukatili kila uchao.
Kwa mujibu wa Takwimu
zilizotolewa mwanzoni mwa mwaka jana zinazoonyesha kuwa watoto milioni 2.5
wamekuwa yatima baada ya wazazi wao kufariki dunia kutokana na ugonjwa wa
Ukimwi na wakati huohuo, watoto wa kike watatu kati ya 10 wamebainika kufanyiwa
ukatili wa kingono kabla ya kufikisha miaka 18.
Hakika, idadi hii ya watoto wanaoishi katika mazingira magumu inatisha. Sisi tunaona kwamba sasa kuna kila sababu kwa serikali na jamii nzima kutafuta namna bora ya kuwasaidia watoto hawa kwani vinginevyo, athari zake zinaweza kuwa kubwa kwa taifa kuliko inavyoweza kudhaniwa.
Hakika, idadi hii ya watoto wanaoishi katika mazingira magumu inatisha. Sisi tunaona kwamba sasa kuna kila sababu kwa serikali na jamii nzima kutafuta namna bora ya kuwasaidia watoto hawa kwani vinginevyo, athari zake zinaweza kuwa kubwa kwa taifa kuliko inavyoweza kudhaniwa.
"Maisha
ya mjini ni magumu sana. Mtu kulala nje, kwenye baridi na mara nyingine
unanyeshewa mvua. Kuna wakati unaweza kuamka asubuhi na kukuta mwenzenu amekufa,"
Anasema mmoja ya watoto hao, msichana mwenye umri wa miaka 16, anasema wengine huishia
kuuza miili yao ili kupata fedha za kununua chakula kabla ya kuanza kutafakari
namna ya mahala pa kulala na usalama wao kimwili na kiakili.
Naye
Mkurugenzi wa Asasi isiyokuwa ya kiserikali yenye usajiri No. ooNGO/08317
inayojishughulisha na kutoa Elimu ya Mazingira kwa wananchi wanaozunguka migodi
pamoja na wafanyakazi wa migodini Bw Ashraf Omary amekiri kuwa athari za kuwapo kwa watoto wanaoshi katika
mazingira hatarishi ni kubwa kwa taifa na hivyo, wakati jitihada za kukabiliana
na visababishi vya kuwapo kwa watoto hao zikiendelea kufanywa, upo ulazima pia
wa kuhakikisha kwamba watoto hawa waliopo mitaani wanapatiwa upendo na huduma
zote kama ilivyo watoto wengine.
”Ikumbukwe kuwa, ikiwa watoto wa mitaani wataendelea kuachwa wajitafutie wenyewe maisha yao, ni dhahiri kwamba nao hawatakuwa na upendo kwa jamii inayowazunguka pindi watakapokuwa watu wazima na hatimaye kuishia kuwa wakabaji pasina kuwa na huruma maana hawakupata upendo na huruma kwa jamii wangali wadogo” Alisisitiza Ashraf Omary
”Ikumbukwe kuwa, ikiwa watoto wa mitaani wataendelea kuachwa wajitafutie wenyewe maisha yao, ni dhahiri kwamba nao hawatakuwa na upendo kwa jamii inayowazunguka pindi watakapokuwa watu wazima na hatimaye kuishia kuwa wakabaji pasina kuwa na huruma maana hawakupata upendo na huruma kwa jamii wangali wadogo” Alisisitiza Ashraf Omary
Akizungumza
na watoto hao mara baada ya kumaliza kula chakula cha jioni Mathias Canal alisema kuwa Katika
kukabiliana na swala hili ni muhimu serikali kukabiliana na changamoto ya
umasikini uliokithiri nchini Tanzania ndio njia pekee ya kunususru Taifa kuwa
na tegemezi wengi tena wenye chuki na hasira na jamii yao kwa kukosekana upendo
wa dhati.
MWISHO
Good.Keep it up
ReplyDeleteGood.Keep it up
ReplyDeleteHappy Birthday brother
ReplyDelete