Katibu
Msaidizi Mkuu wa Idara ya Utawala ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Bw.
Kirumbe Ng’enda akisisitiza jambo mbele ya wanachama wa Shirikisho la
Vyuo vya Elimu ya Juu wa Chama hicho(hawapo pichani) wakati wa Kongamano
la kutathmini sekta ya elimu kwa kipindi cha siku 365 za uongozi wa
Rais Dkt. John Pombe Magufuli jana Jijini Dar es Salaam.Kutoka kushoto
ni Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho hilo Bw. Hamid Saleh Mhina na Katibu
Msaidizi wa Shirikisho Bw. Daniel Zenda.
Makamu
Mwenyekiti wa Shirikisho hilo Bw. Hamid Saleh Mhina akizungumza jambo
katika wa Kongamano la kutathmini sekta ya elimu kwa kipindi cha siku
365 za uongozi wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli jana Jijini Dar es
Salaam.
Katibu
Msaidizi wa Shirikisho la Vyuo vya Elimu ya Juu Tanzania ambaye pia kwa
sasa anashikiria nafasi ya Katibu Mkuu wa Shirikisho hilo, Bw. Daniel
Zenda akifafanua jambo wakati wa Kongamano la kutathmini sekta ya elimu
kwa kipindi cha siku 365 za uongozi wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli
jana Jijini Dar es Salaam.Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Shirikisho
hilo Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Imani Matabula na Makamu Mwenyekiti wa
Shirikisho hilo Taifa, Bw.Hamid Saleh Mhina
Katibu wa
Hamasa wa Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu Tanzania
ambaye pia ndiye alikuwa Mratibu wa Kongamano la kutathmini sekta ya
elimu kwa kipindi cha siku 365 za uongozi wa Rais Dkt. John Pombe
Magufuli, Ndugu Mgwanwa Nzota akielezea jambo wakati wa Kongamano hilo
jana Jijini Dar es Salaam
Mwenyekiti
wa Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu, Mkoa wa Dar es
Salaam Bw. Imani Matabula akizungumza wakati wa Kongamano la kutathmini
sekta ya elimu kwa kipindi cha siku 365 za uongozi wa Rais Dkt. John
Pombe Magufuli jana Jijini Dar es Salaam.Kutoka kulia ni Katibu Msaidizi
wa Shirikisho hilo Taifa, Daniel Zenda, mgeni rasmi katika kongamano
hilo ambaye pia ni mjumbe wa Halamshauri Kuu ya Taifa ya Chama cha
Mapinduzi (Mnec) Kirumbe Ng’enda na Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho hilo
Taifa, Hamid Saleh Mhina.
Mgeni
rasmi katika Kongamano la kutathmini sekta ya elimu kwa kipindi cha siku
365 za uongozi wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Bw. Kirumbe Ng’enda
akiteta jambo na Katibu Msaidizi wa Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo vya
Elimu ya Juu Tanzania Bw. Daniel Zenda (kulia) wakati wa kongamano hilo
jana Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya
wanachama wa Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu Tanzania
wakichangia mada wakati wa Kongamano la kutathmini sekta ya elimu kwa
kipindi cha siku 365 za uongozi wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli jana
Jijini Dar es Salaam.
Kutoka
kushoto ni Mtendaji wa Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu
Taifa, Bi. Deborah Charles, Mwenyekiti wa Shirikisho hilo Mkoa wa Dar es
Salaam Bw. Imani Matabula na Mgeni rasmi (Mnec) Kirumbe Ng’emba
wakiandika hoja zilizoibuliwa na washiriki wa Kongamano la kutathmini
sekta ya elimu kwa kipindi cha siku 365 za uongozi wa Rais Dkt. John
Pombe Magufuli lililofanyika Jijini Dar es Salaam jana.
Baadhi ya
watendaji wa Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu Tanzania
(waliokaa) wakiwa katika picha ya pamoja wanachama wa Shirikisho hilo
kutoka vyuo mbalimbali vya Jijini Dar es Salaam baada ya Kongamano la
kutathmini sekta ya elimu kwa kipindi cha siku 365 za uongozi wa Rais
Dkt. John Pombe Magufuli kumalizika jana Jijini Dar es Salaam.
SHIRIKISHO
la wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu wamepongezwa kwa hatua ya
kuanzisha jukwaa linalowakutanisha baina yao na viongozi wa Chama na
Serikali ili kupata fursa ya kufahamu kinachoendelea na kutoa ushauri.
Pongezi
hizo zimetolewa jana Jijini Dar es Salaam na Mjumbe wa Halmashauri Kuu
ya Taifa (NEC) ya Chama cha Mapinduzi Kirumbe Ng’enda alipokuwa mgeni
rasmi katika Kongamano la kutathmini siku 365 za uongozi wa Mhe. Raios
Dkt. John Pombe Magufuli katika Sekta ya elimu.
Ng’enda
amesema kuwa mbinu hiyo ya kuwaita na kukaa nao pamoja viongozi wa
kiasiasa na Serikali kutasaidia sana kwa makada wa Chama kujua shughuli
mbalimbali za maendeleo nhivyo kuwaweka katika hali nzuri ya kujibu
mashambulizi pindi yanapojitokeza.
“Ni
likuwa naongea na Katibu wenu Zenda ameniambia kuwa huu utaratibu wa
kukutana na viongozi utakuwa endelevu, ni vyema ni waambie tu hatua hiyo
ni muhimu sana na sina budi kuwapongeza kwa ubunifu huo.”Alisema
Ng’enda.
Naye
Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho hilo amesema kuwa wao kamashirikisho
wamejipanga vyakutosha kuahakikisha sasa wanakuwa mstari wa mbele
kukisaidia chama na Serikali kwa rasilimali watu ipo ya kutosha
kufanikisha azma hiyo.
Alitumia
wasaa huo kuwaomba wanachama wote wa Shirikisho hilo nchini kuwa karibu
na wanafunzi wenzxao na kushirikiana nao katika shida na raha kwani kwa
kufanya hivyo ndiyo utendaji unaotakiwa katika awamu hii ya Mhe. John
Pombe Magufuli.
Kwa
upande wake Katibu Msaidizi wa Shirikisho hilo Daniel Zenda alisema kuwa
wao kama Shirikisho ni wajibu wao wa kukishauri Chama cha ili kuleta
matokeo chanya na kuongeza kuwa lengo la Kongamano hilo ni kufanya
tathmini ya namna Serikali ya awamu ya Tano chini ya Uongozi wake Rais
Dkt. John Pombe Magufuli ilivyotekeleza ahadi yake katika sekta ya Elimu
ndani ya mwaka mmoja.
Aidha
Zenda alitumia fursa hiyo pia kumpa pongezi Rais John Magufuli kupitia
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako kwa
kusikiliza kilio cha wanafunzi hali hiliyopelekea kurekebisha baadhi ya
vigezo kwa waombaji wa mikopo.
Zenda
amesema kuwa inatia faraja kuona siku moja baada ya Shirikisho kutoa
tamko kuhusu masula mbalimbali yanayohusu mikopo ya elimu ya juu, Waziri
mwenye dhama alichukua hatua ambazo kimsingi zimeonyesha ni namna gani
Serikali yetu ilivyo sikivu.
“Kwa
dhati kabisa naipongeza Serikali ya Rais Magufuli kwani imeonyesha
usikivu wa hali ya juu,lakini pia kipekee nimpongeze mama yetu Mhe.
Waziri wa Elimu Profesa Ndalichako kiukweli ameonyesha kuwa ni kiongozi
anayejali wanyonge”. Alisema Zenda.
No comments:
Post a Comment