Mkurugenzi
wa Shirika la Hifadhi ya Jamii NSSF,Prof. Godius Kahyarara akizungumza
na Waandishi kuhusiana na mradi wa Jengo la NSSF (Mzizima Tower) .
Baadhi ya Watumishi wa Shirika hilo wakiwa katika picha ya pamoja.
Na Anthony John blog Jamii
Shirika
la Taifa la Hifadhi ya Jamii limekamilisha mradi wa Jengo refu Afrika
Mashariki-Mzizima Tower lililopo barabara ya Azikiwe na Mkwepu Dar es
salaam.
Akizungumza
na Waandishi wa Habari katika Makao Makuu ya Shirika hilo,Mkurugenzi wa
Shirika hilo Prof. Godius Kahyarara amesema Jengo hilo lipo hatua za
mwisho za ukamilishaji wa ujenzi ambalo litakuwa na ghorofa 30 za makazi
na 32 za Biashara.
Pia
amesema Jengo hilo litakuwa na hoteli ya Nyota 5 na nyumba za makazi kwa
ajili ya kuuza na kupangisha,Jengo linatarajiwa kukamilika mwakani
2017.Aidha Shilika hilo limesaini makubaliano na atakayekuwa muendeshaji
wa Hoteli hiyo itakayokuwa katika Jengo la Mzizima na kutarajiwa kuanza
kazi Mara moja baada ya Hoteli hiyo kufunguliwa.
No comments:
Post a Comment