Willy Nyamitwe, akihojiwa na mwanahari wa RFI Kifaransa Sonia Rolley, hivi karibuni
Serikali
ya Burundi, imeishtumu nchi jirani ya Rwanda kwa kupanga shambulizi
dhidi ya msemaji wa rais Pierre Nkurunziza, Willy Nyamitwe.
Mmoja
wa mlinzi wake aliuawa na mwingine kujeruhiwa katika shambulizi hilo
huku Nyamitwe akijeruhiwa mkononi na kwenda kupata matibabu.
Katika ukurasa wake wa Twitter, Nyamitwe ameandika kuwa anaendelea vema lakini anaomboleza kifo cha mlinzi wake.
Msemaji
wa Polisi nchini humo Pierre Nkurukiye, amesema watu waliokuwa
wamejihami kwa silaha walipata maagizo kutoka Rwanda kumuua Nyamitwe.
Aidha,
amesema baada ya shambulizi hilo wanajeshi wawili wa Burundi wamekamatwa
kwa kuhusika katika shambulizi hilo lililotokea usiku wa kuamkia siku
ya Jumanne.
Licha ya
tuhma hizo, serikali ya Rwanda haijazungumzia tuhma hizo lakini imekuwa
ikikanusha mara kwa mara kuhusika na machafuko nchini Burundi.
Uhusiano kati ya mataifa haya mawili umekuwa mbaya tangu jaribio la mapinduzi nchini Burundi mwaka 2015.
Burundi
pia imekuwa ikiishtumu Rwanda kwa kuwapa mafunzo ya kijeshi wakimbizi
wanaokimbilia katika nchi yake, ili kushambulia utawala wa rais
Nkurunziza.RFI
No comments:
Post a Comment