Issa Kapande `Chef Issa'
Mgahawa
mkubwa unaotoa huduma za chakula cha Kitanzania unaomilikiwa na mpishi
maarufu duniani, Issa Kapande `Chef Issa', umefunguliwa nchini Sweden na
kuvunja rekodi ya dunia.
Mgahawa huo ulizinduliwa na balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mh. Dora Msechu.
Balozi
Msechu alimpongeza Issa Kapande na mkewe kwa kufanikisha kuwapo kwa
mgahawa huo ambao umeweka rekodi kuwa mgahawa mkubwa kuliko yote ya
Kiafrika katika nchi za Ulaya.
Aidha,
alimshukuru Torvald Brahm mwenyeji wa mji huo kwa kumuunga mkono Issa
hadi kufanikisha ndoto yake ya kuwa na mgahawa wa kwanza wa Kiafrika
katika mji wa Trollhattan utakatoa huduma ya chakula cha kitanzania.
Katika
uzinduzi huo ambapo wenyeji wa manispaa hiyo akiwemo Meya na mwenyekiti
wa Trollhattan, Paul Akerlund na msaidizi wake Peter Eriksson
walikuwepo, balozi ambaye ndio kwanza ameanza kazi alielezea
kufurahishwa na juhudi za Kapande.
Alisema
Issa ameonesha njia kwamba inawezekana kwa watu waliopo Ughaibuni sio tu
kuajiriwa, bali kujiajiri katika nyanja mbalimbali.Alisema hilo
linawezekana kutokana na kufuatilia kwa karibu taratibu za wenyeji na
kisha kutumia mafunzo yaliyopo kukamilisha ndoto.
"Ni
dhahiri kuwa, Chef Issa kwa kupitia taaluma yake ya upishi amewezeshwa
kumiliki mgahawa huu hapa Trollhattan,S weden kwa hilo, napenda
tuishangilie na kuipigia makofi Sweden na Trollhattan."Alisema
akimpongeza kijana huyo ambaye pia amewekeza mkoani Mtwara.
Katika
mahojiano, Mpishi Mkuu Issa Kapande alisema mafanikio yake yanatokana na
juhudi kubwa na nia aliyoiweka katika kujifunza na kufundisha wengine
katika mitandao ya wapishi wakuu.
Alisema
akiwa amefanyakazi katika nchi 17 na tayari akiwa na vitega uchumi
nchini alianzia nia ya kuwekeza Sweden mwaka 2009 wakati alipohamia
nchini humo akitokea Uswisi. Alisema alianza kwa kuomba vibali, lakini
mchakato kamili ulianza mwaka 2013."Tulilazimika kufanya utafiti kidogo"
alisema na kuongeza kuwa katika utafiti huo walihoji watu 300 na kujua
mwelekeo hasa wa shughuli yao unastahili kuwaje.
Kapande
ambaye ni mhitimu wa chuo kikuu cha Manchester Metropolitan na Chuo
kikuu cha kimataifa cha menejimenti ya hoteli cha Uswis amesema
amepambana vikali na mkewe hadi kufikia hatua ya kuanzisha mgahawa huo
ambao upo katika eneo la ukubwa wa skwea mita 810.Kapande ambaye mwaka
jana alitwaa tuzo ya dhahabu katika upishi akiwa na timu ya Sweden
magharibi alisema kuna umuhimu mkubwa kwa wapishi wa nyumbani kukubali
kubadilika na kufanya kazi kwa pamoja kwa lengo la kujifunza na kufunza
ili kuwa na aina nyingine ya mapishi katika kuendeleza sekta.
Ndani ya mgahawa huo pia watu mbalimbali watapatiwa taarifa za utalii Tanzania.
Katika
kazi yake ya upishi, amebahatika kuwapikia watu mashuhuri duniani,
baadhi wakiwa Andrew Young, Mchungaji Jesse Jackson, Robert Mugabe (Rais
wa Zimbabwe), Paul Kagame (Rais wa Rwanda), Benjamini Mkapa (Rais
mstaafu wa Tanzania), Raila Odinga (Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya),
Daniel Arap Moi (Rais Mstaafu wa Kenya), Waziri wa Mambo ya Nje wa
Marekani Bi. Hillary Clinton na mumewe Bill Clinton, Mke wa Rais wa
zamani wa Marekani Laura Bush.
Wengine
ni Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein, mwigizaji Chris Tucker, Rais
wa zamani wa Afrika Kusini hayati Mzee Nelson Mandela, Koffie Olomide,
Youssour ndour, Arsene Wenger (Kocha wa Arsenal ya England), Gianluca
Vialli (nyota wa zamani wa Italia aliyewahi kuichezea na kuinoa Chelsea
ya England), Rais wa Congo DRC, Joseph Kabila, Billy Gates na wengine
wengi.BBC
No comments:
Post a Comment