Seneta wa
juu kabisa wa chama cha Democrat, amesema Mkurugenzi wa FBI James Comey
anaweza kuwa amevunja sheria kwa kutangaza kubaini barua pepe mpya
zinazoweza kuwa muhimu kwa uchunguzi dhidi Hillary Clinton
Katika
barua yake kwa Comey, kiongozi wa kundi la wachache Harry Reid, seneta
wa Nevada amemtuhumu kiongozi huyo kwa kuwa na undumilakuwili kwa kuwa
na nia ya kudhibiti wito wa Democrat kujadili kile kinachoelezwa kuwa
uwezekano wa mahusiano kati ya Donald Trump na serikali ya Urusi, na
badala yake Ijumaa iliyopita kutoa taarifa kwa bunge la
Marekani-Congress za ujumbe wa kingono, katika uchunguzi wa Anthony
Weiner, mbunge wa zamani wa New York na mume wa zamani wa msaidizi wake
mkuu wa Clinton Huma Abdidin.
Katika
taarifa hiyo Reid amemwambia kiongozi huyo wa FB kuwa jitihada za wazi
kabisa zenye kuonesha ana nia ya kusaidia upande mmoja wa chama. Aidha
ameongeza kuwa ofisi yake imemuandikia barua hiyo kwa kutanabaisha kuwa
amekiuka sheria iitwayo "Hatch Act", ambayo inawazuia maafisa wa FBI
kutumia mamlaka yao ya kiofisi katika kufanikisha ushawishi katika
chaguzi. Amesema kwa kitendo cha kujiegemeza kwa upande wa chama
amevunja sheria za taifa hilo.
Kutikisika mbio za Ikulu ya Marekani
Comey
amezitikisa mbio za ikulu ya Marekani- White House kwa barua yake kwa
Congress, akiwaeleza wabunge kupatikana kwa barua pepe mpya. Chama cha
Democrat kina wasiwasi uvumbuzi huo mpya unaweza kumpa nguvu mpya
mgombea wa Republican katika juma la mwisho kuelekea uchaguzi wa rais
pamoja na kuwaongezea nguvu wagombea wa useneta na baraza la wawakilishi
katika uchaguzi huo.
Katika
hatua tofauti kufuatia kadhia hiyo mwanasheria mkuu wa zamani Eric
Holder na waendesha mashitka wengine kadha wa kadhia wametia saini barua
inayomkosoa Comey kutokana na kisa hicho cha hivi karibuni cha namna
anavyoshughulikia tuhuma za barua pepe za mgombea Clinton.
Katika
barua hiyo ambayo shirika la habari la Ufaransa la AP imeipata nakala
yake inasema Comey amejitenga na kitenmgo cha sheria pale alipolidokeza
bunge la Marekani juu ya uchunguzi mpya wenye kuhusiana na uchunguzi
mpya kuhusiana na kashfa ya Clinton.
Aidha
barua hiyo vilevile imeeleza maafisa wa Kitengo cha Sheria nchini humo
wameagizwa wasiendelee kujadili uchunguzi unaondelea na kujitenga kabisa
na jambo hilo katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi, kwa lengo la
kuondosha ushawishi wao. Lakini mkurugezi wa FBI alikwisha sema pale
alipozungumza na maafisa wenzanke wa shirika hilo la ujasusi Ijumaa
iliyopita kuwa barua yake kwa bunge la Marekani ipo katika hatari ya
kutoeleweka katika kipindi hiki cha karibu na uchaguzi, lakini alipsawa
kulipa taarifa bunge hilo baada ya awali kulieleza kuwa uchguzi wake
ulifungwa.
DW
No comments:
Post a Comment