Wednesday, November 30, 2016

MD KAYOMBO AFANIKISHA MRADI SHULE YA MATOSA

 Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo amepongezwa na walimu pamoja na wanafunzi wa shule ya sekondari Matosa iliyopo Kata ya Goba , Manispaa ya Ubungo kwa kufanikisha kwa kiasi kikubwa utekelezaji wa mradi wa SEDP II.

Mradi huo unaohusisha ujenzi wa vyumba viwili vya darasa, nyumba za walimu, kisima cha maji, tanki la kuhifadhia maji pamoja na vyoo upo katika hatua nzuri ya kukamailika kutokana na juhudi pamoja na utendaji kazi uliotukuka wa Mkurugenzi Kayombo akishirikiana na watumishi wa Manispaa hiyo.

Akizungumza na mtandao wetu mwalimu Mkuu wa shule hiyo alisema amefurahishwa na juhudi zinazofanywa na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo za kuleta maendeleo kwa wananchi na kwenda sambamba na kauli mbiu ya Rais John Pombe Magufuli ya Hapa Kazi Tu.

"Napenda kutoa shukrani Kwa Serikali kwa kuuleta mradi wa SEDP II katika shule yetu, pia napenda kutoa shukrani za dhati kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg. John Lipesi Kayombo kwa juhudi zake anazozifanya mpaka mradi umefika hatua hii, kwa kweli ametusaidia sana, mungu ambariki", alisema Mwalimu mkuu.

Wakati huo huo wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo wamempongeza Mkurugenzi Kayombo kwa kazi nzuri aliyofanya mpaka kuweza kufanikisha kupatikana kwa maji pamoja na madarasa, vyoo, tanki la maji na nyumba za walimu.

No comments:

Post a Comment