Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Willim Lukuvi anaendelea
na ziara ya siku tatu katika mkoa wa Kigoma ambapo amefungua rasmi
Baraza la Ardhi na Nyumba la Mkoa wa Kigoma pamoja na kutatua migogoro
ya ardhi ya wananchi wa Kigoma.
Wananchi
hao wamempongeza Mhe. Waziri kwa hatua anazozichukua katika kumaliza
migogoro yao ya ardhi na kuwajengea Baraza la Ardhi na Nyumba ambalo
jipya na lililo na viwango kushinda mengine yote hapa nchini.
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Willim Lukuvi akifungua
Baraza la Ardhi na Nyumba la Mkoani Kigoma, Kushoto ni Mbunge wa Kigoma
Mjini Mhe. Zitto Kabwe na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe.Brigedia
Jenerali Emanuel Maganga.
Jengo jipya la Baraza la Ardhi na Nyumba la Mkoani Kigoma.
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Willim Lukuvi akiongea na
wananchi wa Kigoma Mjini na kutatua migogoro yao ya ardhi.
No comments:
Post a Comment