Monday, November 7, 2016

Mali: shambulizi dhidi ya msafara wa Minusma

media
Askari wa Minusma, kikosi cha Umoja wa Mataifa Mission nchini Mali, katika mji wa Timbuktu, Septemba 19, 2016.

Nchini Mali, siku moja baada ya kifo cha askari wa Ufaransa aliyeuawa katika mlipuko wa bomu la ardhini kaskazini mwa nchi hiyo, shambulizi jingine jipya lililenga Jumapili hii kikosi cha Umoja wa Mataifa kiliyotumwa nchini humo. Askari mmoja alipoteza maisha na saba kujeruhiwa, huku watatu wakiwa ni katika hali mbaya.

Shambulizi hili lilitokea kaskazini mwa mji wa Douentza, karibu na kijiji cha Bambara Maoudé katikati mwa Mali. Msafara wa magari ya Umoja wa Mataifa, uliyokua ukishindikizwa na askari wa kulinda amani, ulikanyaga mabomu mengi ya ardhini. Shambulizi hili lilifuatiwa na urushianaji risasi.

Inaarifiwa kuwa washambuliaji hao walikua wakisubiri msafara huo. Askari walijibu haraka, na kuwatimua washambuliaji hao.

Umoja wa Mataifa ulituma helikopta zake za kivita, lakini kutokana na hali ya iliyokua ukijiri katika eneo la shambulizi, helikopta hizi iliwasafirisha majeruhi hadi hospitali. Kwa mujibu wa Minusma, askari wa kikosi hiki kutoka Togo alifariki muda mfupi baada ya kuwasili kwa askari wengine waliokuja kusaidia, askari wengine saba walijeruhiwa, ikiwa ni pamoja na watatu ambao wako katika hali mbaya. Wote walisafirishwa katika mji wa Timbuktu.

Minusma imebaini kuwa shambulizi hili ni tata. Katikati na kaskazini mwa Mali, mashambulizi kwa kutumia mabomu ya ardhini yamekithiri na ni moja ya mbinu ambayo inatumiwa na makundi ya kigaidi yenye silaha.RFI

No comments:

Post a Comment