Waziri wa
Afya wa Zanzibar Mh.Mahamud Thabit Kombo akizungumza na viongozi
mbalimbali wa NHIF kuhusu kujifunza kutokana na uzoefu wa kuendasha
Mfuko wa bima ya afya, katika ziara ya mafunzo makao makuu ya NHIF jana
jijini Dar es Salaam.kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya NHIF, Bi. Anne
Makinda (Spika Mstaafu).
Mwenyekiti
wa Bodi ya NHIF, Bi. Anne Makinda (Spika Mstaafu) akitoa maelezo mafupi
kuhusu shughuli za Mfuko jana makao makuu ya mkuko jijini Dar es
Salaam. Kushoto ni Waziri wa Afya wa Zanzibar Mh.Mahamud Thabit Kombo.
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Bw. Bernard Konga akitoa maelezo mafupi kuhusu
shughuli za Mfuko jana makao makuu ya mkuko jijini Dar es Salaam. Kulia
ni Waziri wa Afya wa Zanzibar Mh.Mahamud Thabit Kombo.
Meneja
Wanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Elentruda Mbodoro
akitoa walezo mafupi kwa Waziri wa Afya wa Zanzibar Mh.Mahamud Thabit
Kombo kuhusu utunzaji wa nyaraka za wanacha wa mfuko huo jana jijini
Dar es Salaam.
Waziri wa
Afya wa Zanzibar Mh.Mahamud Thabit Kombo akiwa katika picha ya pamoja
na viongozi mbalimbali wa NHIF jana makao makuu jijini Dar es Salaam
Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii
Mfuko wa
Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umepokea ugeni kutoka Wizara ya Afya ya
Zanzibar katika ziara ya mafunzo iliyoongozwa na Mh.Mahamud Thabit Kombo
ambaye ni Waziri wa Afya wa Zanzibar.
Katika
ziara hiyo, yenye lengo la kushiriki uzoefu wa utekelezaji wa shughuli
za Mfuko huo, Waziri na timu yake walipata melezo na kujionea shughuli
mbalimbali za Mfuko huo.
Akizungumza
wakati wa ziara hiyo, Mh.Kombo alisema “tunahitaji kujifunza kutokana
na uzoefu wenu wa kuendasha Mfuko wa bima ya afya, hatukuona haja ya
kwenda mbali kwani tuna kaka na dada zetu hapa karibu na wana uzoefu wa
kutosha”.
Mh. Kombo
alisema kuwa Wizara ya Afya ya Zanzibar ina ushirikiano mkubwa sana na
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto na
kusisitiza kuwa Wizara hizi zinafanya kazi kwa karibu sana na hii
inasaidia kufanikisha maendeleo ya sekta ya afya kwa pande zote.
Akiwakilisha
mada ya Utekelezaji wa shughuli za Mfuko,Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF
Bw. Bernard Konga aliongelea umuhimu wa Bima ya Afya katika maendelea ya
sekta ya afya nchini na kuanisha utekelezaji wa majukumu ya Mfuko huo
ambapo alielezea pia mifumo imara ya uendeshaji wa Mfuko ikiwemo ya
Tehama lakini pia mifumo ya kubaini udanganyifu ili kuudhibiti.
Naye
Mwenyekiti wa Bodi ya NHIF, Bi. Anne Makinda (Spika Mstaafu) lielezea
umuhimu wa Mfuko kujipanga kimuuondo katika kuhakikisha unaweza kufikia
azma ya Serikali ya kuhakikisha afya bora kwa wote. “Pamoja na mambo
mengine, elimu kwa umma ni suala la msingi sana katika utekelezaji wa
shughuli za Mfuko na kuwapa nafasi wadau kuuliza na kujibiwa hoja
zao”alisema.
No comments:
Post a Comment