Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Angellah J. Kairuki
amekanusha taarifa inayosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa
serikali ina mpango ya kuhakiki namna watumishi wake wanavyotumia
mishahara yao.
Waziri
Kairuki kupitia akaunti yake ya matandao wa Twitter amesema kuwa
taarifa hiyo ni ya uongo na kuwataka wananchi kuipuuza kwani ina lengo
la kupotosha umma.
“Kuna
taarifa ya uongo inayosambazwa mtandaoni kwamba “kutakuwa na zoezi la
kuhakiki watumishi wa umma wanavyotumia mishahara yao”.Ipuuzieni.”
“Si
dhamira wala desturi ya Serikali yetu kuingilia maisha binafsi ya
watumishi wa umma hususan matumizi ya mishahara yao.Puuzieni uzushi
huo.”
Taarifa
hiyo imemnukuu Waziri Kairuki kuwa serikali baada ya kukamilisha
uhakiki wa vyeti kwa watumishi wake, wataanza uhakiki wa jinsi watumishi
wa umma wanavyotumia mishahara yao ili kurejesha maadili kwa watumishi
wa umma.
Kuhusu
uhakiki wa vyeti kwa watumishi wa serikali, Rais Magufulii alisema kuwa
lengo la zoezi hilo si kuwafukuza watumishi lakini ni kujiridhidha kama
malipo yanayofanyika kwa watumishi hao yanalandana na viwango vya elimu
wanavyoeleza kuwa wanavyo.
No comments:
Post a Comment