Kamati
ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetoa onyo kali
kwa kituo cha Televisheni cha Clouds sambamba na kukifungia kwa kipindi
kwa miezi mitatu kipindi cha Take One kinachorushwa na Kituo hicho.
Makamu
mwenyekiti wa kamati hiyo Method Mapunda amesema sababu ya kukifungia
kipindi hicho ni kutokana na ukiukwaji wa kanuni za utangazaji za mwaka
2005, kwa kumhoji na kurusha kipindi cha mtu kinachohamasisha biashara
ya ngono, kuingilia faragha ya mtu na kutolinda maadili ya watoto.
“Clouds
tv inapaswa kukitathimini upya kipindi hicho kwa lengo la kupata njia
bora ya kukiendesha na kupeleka mapendekezo TCRA kwa ajili ya
kujiridhisha kabla ya kipindi hicho kufunguliwa,”alisema mapunda.
Mahojiano
yaliyopekea kipindi hicho kufungiwa ni kati ya mtangazaji wa kipindi
hicho Zamaradi Mketema na Gift Stanford Maarufu kama ‘Gigy Money’ na
yalirushwa Agost 09 saa 3.00 usiku na kurudiwa kesho yake saa 7.00
No comments:
Post a Comment