Wanawake wanne na wanaume tisa wamefikishwa mahakamani mjini Dodoma na kusomewa mashtaka ya mauaji ya watafiti wa Chuo cha Utafiti wa Udongo na Maendeleo ya Ardhi kilichopo Selian mkoani Arusha.
Mbele
ya Hakimu Mkazi, Joseph Fovo washtakiwa hawakutakiwa kujibu chochote
kwa kuwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma haina mamlaka kisheria
kusikiliza kesi hiyo isipokuwa Mahakama Kuu.
Wanadaiwa
kuwaua Nicas Mag- azine, Theresia Nguma na Faraji Mafuru, Oktoba Mosi
kwenye Kijiji cha Iringa Mvumi wilayani Chamwino.
Wakili
wa Serikali, Beatrice Nsana aliwasomea mashtaka hayo jana akidai
walitenda kosa hilo la jinai kinyume na kifungu cha 196 na 197 cha
Sheria ya Kanuni ya Adhabu na marekebisho yake ya mwaka 2002.
Washtakiwa
hao ni Cecilia Mwalu, Dorca Mbehu, Edna Nuno, Grace Masaulwa, Juma
Madeha, Albert Chimanga, Sosteness Mseche, Julius Chimanga, David
Chimanga, Lazaro Kwanga, Yoramu Samamba, Edward Lungwa na Simon Samamba,
wote wakazi wa Kijiji cha Iringa Mvumi.
Kesi hiyo namba 36/2016 iliahirishwa hadi Oktoba 31. Nsana alidai upelelezi haujakamilika.
Kesi hiyo namba 36/2016 iliahirishwa hadi Oktoba 31. Nsana alidai upelelezi haujakamilika.
No comments:
Post a Comment