Waziri
Mkuu wa Canada Justin Trudeau na viongozi wa Umoja wa Ulaya Jumapili
(30.10.2016) hatimae wamesaini makubaliano ya kihistoria ya biashara
yaliyochukuwa miaka saba kutayarishwa na yaliyokuwa nusura
yasambaratike.
Waziri
Mkuu wa Canada Justin Trudeau na viongozi wa Umoja wa Ulaya Jumapili
(30.10.2016) hatimae wamesaini makubaliano ya kihistoria ya biashara
yaliyochukuwa miaka saba kutayarishwa na ambayo yalikuwa nusura
yasambaratishwe na mkoa mmoja mdogo wa Ubelgiji.
Hafla ya
kusainiwa kwa makubaliano hayo mjini Brussels iliahirishwa kutoka
Alhamisi baada ya mkoa wenye wakaazi milioni 3.5 tu wanaozungumza
Kifaransa wa Wallonia awali kutumia kura yake ya turufu kupinga
makubaliano hayo yenye taathira kwa zaidi ya watu milioni 500 wa Ulaya
na wananchi milioni 35 wa Canada.
Shangwe
na vifijo viliripuka wakati Trudeau akisaini makubaliano hayo pamoja na
Rais wa Barazan la Umoja wa Ulaya Donald Tusk, Mkuu wa Halmashauri Kuu
ya Umoja wa Ulaya Jean -Calude Juncker na Waziri Mkuu wa Slovakia Robert
Fico ambaye nchi yake inashikilia urais wa kupokezana wa umoja huo.
Awali
waandamanaji walipenya safu ya polisi wa kuzuwia fujo na kumwaga rangi
nyekundu kwa makao makuu ya Umoja wa Ulaya huku wanaharakati wakicheza
ngoma na kutowa kauli mbiu zenye kupinga makubaliano hayo Kabambe ya
Kiuchumi na Biashara kati ya Umoja wa Ulaya na Canada.
Kuanza
kwa mkutano huo wa kilele kumezidi kucheleweshwa wakati ndege ya Trudeu
ilipolazimika kurudi nyumbani kwa muda kutokana na matatizo ya kufundi.
Ushuru kuondolewa
Makubaliano
hayo ya CETA yanaondowa ushuru wa forodha kati ya pande hizo mbili na
kuliunganisha soko la pamoja la Ulaya na nchi yenye kushikilia nafasi ya
kumi kwa kuwa na uchumi mkubwa duniani.
Sakata
hilo la Ubelgiji liliibuwa tahadhari kuhusu kuaminika kwa Umoja wa Ulaya
kama mshirika wa kibiashara wakati huku ikiwa imezongwa na hatua ya
kufadhaisha ya Uingereza kujitowa Umoja wa Ulaya,mzozo wa wahamiaji na
kuibuka upya kwa Urusi.
Baada ya
mazungumzo za miaka mingi makubaliano hayo yalikuwa nusura yasambaratike
na Trudeu alikubali Ijumaa usiku kwenda Brussels baada ya Wallonia
kukubali hatimae kujiunga na mikoa iliobakia ya Ubelgiji na nchi
nyengine wanachama 27 za Umoja wa Ulaya kuidhinisha makubaliano hayo.
Nchi zote zilitakiwa ziuidhinishe
Mkataba
huo ulikuwa ukitaka nchi zote za Umoja wa Ulaya ziuidhinishe na katika
baadhi ya kesi kama vile Ubelgiji serikali za mikoa zilitakiwa pia
kufanya hivyo na hiyo kutowa fursa kwa mkoa wa Wallonia kuwa na uwezo wa
kura ya turufu.
Mkoa huo
wa Wallonia ulihimili shinikizo kubwa kwa wiki mbili kutoka pande zote
mbili hadi pale iliporidhiwa madai yake katika maslahi ya kilimo na
hakikisho kwamba wawekezaji wa kimataifa hawatoweza kuzilamisha serikali
kubadilisha sheria.
Wasi wasi
wa kudhoofika kwa mkoa huo ulioendelea kiviwanda ulioko kusini mwa
Ubelgiji unaonyesha wasi wasi wa jumla ulioko barani Ulaya kuhusu
utandawazi halikadhalika hofu miongoni mwa wanaharakati kwamba
makubaliano ya aina hiyo yanadhoofisha ulinzi kwa mlaji , jamii na
mazingira.
DW
No comments:
Post a Comment