Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu L. Nchemba (Mb) akizungumza wakati
wa mkutano na vyombo vya habari mkoani Dodoma kuhusu mwenendo wa zoezi
linaloendelea la usajili wa Vitambulisho vya Taifa kwa Watumishi wa
Umma. Katikati ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mh. Angellah J. Kairuki (Mb) na Bi.
Rose Mdami, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Hifadhi Hati,
akimwakilisha Kaimu Mkurugenzi Mkuu NIDA
Katikati
ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu L. Nchemba (Mb)
Akisisitiza jambo wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari kuhusu
zoezi la kusajili watumishi wa Uma nchi nzima. kulia ni Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mh.
Angellah J. Kairuki (Mb) na kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi Meja Jenerali Projest Rwegasira
Baadhi ya
waandishi wa Habari nchini wakisikiliza kwa makini ufafanuzi unaotolewa
na Mawaziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora; kuhusu usajili wa Vitambulisho vya
Taifa kwa watumishi wa Umma zoezi linaloendelea nchi nzima
Baadhi ya
waandishi wa Habari walioshiriki mkutano wa tathmini ya mwenendo wa
Usajili Vitambulisho vya Taifa kwa watumishi wa Umma; mkutano
uliofanyika ukumbi wa Kambarage, jengo la Hazina Dodoma
Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu L. Nchemba (Mb) akiweka saini
kitabu cha wageni alipotembelea ofisi za Usajili za Mamlaka ya
Vitambulisho vya Taifa mkoani Dodoma, kukagua shughuli za usajili
Watumishi wa Umma kabla ya kuzungumza na waaandishi wa habari kutoa
tathmini ya mwenendo wa zoezi hilo
Waziri
akipokea maelezo ya namna shughuli za usajili zinavyo ratibiwa na ofisi
ya usajili Wilaya ya Dodoma Mjini ; alipofanya ziara ya ukaguzi na
kukutana na viongozi na watumishi wa Umma waliofika kupata huduma.
Serikali
imewataka watumishi wote nchini walioajiriwa na Serikali, yakiwemo
mashirika ya Dini na Taasisi nyingine ambazo haziko kwenye orodha ya
malipo ya mishahara ya Serikali lakini zinapata ruzuku kutoka
Serikalini; kuwa wamesajiliwa katika zoezi la Vitambulisho vya Taifa
kwa Watumishi wa Umma linaloendelea kote nchini, kufikia Oktoba 31,
2016.
Agizo
hilo limetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mh. Angellah J. Kairuki (Mb)
alipozungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma, katika mkutano wa
pamoja ulioitishwa kati ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na Waziri
ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Bi
Kairuki amesisitiza; “waajiri na watumishi watakaoshindwa kutekeleza
zoezi hili watachukuliwa hatua stahiki kwa mujibu wa sheria, kanuni na
taratibu zilizopo”
Akifungua
mkutano huo uliolenga kutoa tathmini ya mwenendo wa zoezi
linaloendelea la Usajili wa Vitambulisho vya Taifa kwa Watumishi wa Umma
lilioanza nchi nzima tangu Oktoba 03, 2016, Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi Mh. Mwigulu L. Nchemba (Mb) amesema mpaka sasa Mamlaka ya
Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imefanikiwa kusajili zaidi ya asilimia
50% ya watumishi wote nchi nzima na baadhi ya mikoa kukamilisha usajili
kwa zaidi ya asilimia 95%. Ameutaja mkoa wa Geita kuwa mkoa unaoongoza
kwa kufanya vizuri katika zoezi hilo
Amesema
pamoja na kuwepo kwa changamoto mbalimbali zilizokwamisha zoezi hilo
kukamilika kwa wakati uliopangwa; Wizara yake kwa kushirikiana na Ofisi
ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, wameamua kuongeza muda wa
kukamilisha zoezi hilo kwa wiki mbili zaidi hadi Oktoba 31, 2016.
Amewataka
watumishi kuondokana na upotoshwaji unaofanywa na baadhi ya watumishi
kwamba zoezi hilo limelenga kuhakiki vyeti na badala yake wajitokeze kwa
wingi kusajiliwa kwani Serikali imelenga kuunganisha taarifa za mfumo
wa mishahawa wa Serikali na NIDA, ili mbali na kutatua tatizo la
watumishi hewa; kupitia mfumo huu wa kielektroniki unaomtambua mtu kwa
alama zake za kibaiolojia kuwa na maslahi mapana kwa taifa na kwa
watumishi; kwa kuunganisha mifumo mingine ya Serikali ukiwemo mfumo wa
Kodi, mifuko ya Hifadhi za Jamii, Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu, Bima
ya Afya, Uhamiaji, RITA Na Benki ili kutoa manufaa mapana kwa mtumishi.
Amelipongeza
Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwa kuwezesha kusambazwa kwa vifaa vya
usajili nchi nzima, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Taasisi na Mashirika yote ya
Serikali waliojitoa kufanikisha zoezi la Usajili.
No comments:
Post a Comment