Mahakama
ya juu ya nchini Angola imemuagiza rais wa nchi hiyo, Jose eduardo dos
Santos kujibu tuhuma kuhusu sababu za kumteua binti yake Isabel dos
Santos kuongoza kampuni ya taifa ya mafuta ya Sonangol.
Dos
Santos alimteua binti yake huyo Bilionea kama mtendaji mkuu wa kampuni
hiyo a taifa ya mafuta ya Sonangol mnamo mwezi Juni mwaka huu, na mara
baada ya uteuzi mwanamama huyo aliahidi kuifanyia mabadiliko makubwa
kampuni hiyo kiutendaji na kiuzalishaji ikiwa ni sehemu ya mkakati wake
wa kukabiliana na matokeo ya kukatisha tamaa kwenye bei ya mafuta.
Kulingana
na nyaraka za mahakama hiyo ya juu ambazo shirika la habari la Reuters
limepata naka zake, rais Eduardo Santos ametakiwa kujibu tuhuma hizo.
Mahakama hiyo imeanza kuyafanyia kazi maombi ya shauri lililowasilishwa
mahakamani hapo na wanasheria 14 wa Angola wanaomtuhumu rais kwa
kuendekeza undugu na kuvunja sheria ya uaminifu ya nchi hiyo.
Hata
hivyo, si rais mwenyewe, msemaji kutoka kitengo cha mawasiliano cha
Ikulu ama Isabel mwenyewe hawakupatikana mapema wala kupokea simu
kuzungumzia kuhusu mwito huo wa mahakama. Isabel, aliteuliwa kuchukua
mamlaka hayo mara baada ya hatua ya kushtukiza ya rais ya kuvunja bodi
ya Sonangol.
Miongoni
mwa hatua ambazo Isabel aliahidi kuzichukua dhidi ya kampuni hiyo ni
pamoja na kuigawanya kampuni hiyo na kuwa na vitengo vitatu, ambavyo
kimoja kitaangazia zaidi masuala ya uzalishaji, kitengo cha usafirishaji
na vifaa na kitengo kitakachohusika na mikataba.
Uteuzi
huo ulichukuliwa na baadhi ya wachambuzi kama hatua ya rais dos Santos
ya kujitengenezea njia ya urithi kwa ukoo wake, iwapo atatekeleza azma
yake aliyotangza mwezi Machi ya kuondoka madarakani ifikapo mwaka 2018,
ikiwa ni mwaka mmoja baada ya uchaguzi mkuu, ingawa wengine wanasema
inawezekana alikuwa akimaanisha kuleta mabadiliko ndani ya kampuni hiyo.
Angola,
ambayo ni mwanachama wa muungano wa nchi zinazosafirisha mafuta nje,
OPEC, kwa sasa ni mzalishaji mkubwa zaidi wa mafuta barani Afrika, baada
ya Nigeria kuanguka kiuzalishaji kutokana na mashambulizi ya wanamgabo
dhidi ya miudombinu ya mafuta na matatizo mengine. Hata hivyo
inakabiliwa na changamoto kubwa ya kuanguka kwa bei ya mafuta, hatua
iliyoifanya nchi hiyo kupunguza matumizi.
Isabel
Santos, ambaye ni binti wa kwanza wa Rais santos, ametajwa kwenye jarida
la FORBES kama mwanamke tajiri zaidi barani Afrika, ambaye pamoja na
sasa kuwa mtendaji mkuu kwenye kampuni hiyo ya taifa ya mafuta, bado
amewekeza kwa kiasi kikubwa kwenye sekta za mawasiliano, benki,
televisheni ya setilaiti na hata kwenye michezo. Utajiri wake unafikia
Dola za kimarekani, Bilioni 3.2.
Mwandishi
wa habari Rafael Marques wa Angola ambaye amekuwa akifuatilia mzizi wa
utajiri wa Isabel kwa miaka mingi anasema kwamba baba yake Jose Eduardo
dos Santos amekuwa na dhima kubwa katika kumjengea utajiri huo. Ameiambi
DW kwamba kila alichotaka Isabel baba yake alihakikisha anakipata.
Anasema, aliwahi hata kumpa madaraka ya kusimamia fedha katika mikataba
mikubwa ya serikali, ingawa Isabel mwenyewe anapinga tuhuma hizo.
Hata
hivyo, baadhi ya watu wanamuangalia Isabel Dos Santos kama mfano wa
wafanyabiashara barani Afrika ambao wametoa nafasi za ajira
zinazohitajika kwa kiasi kikubwa, katika taifa hilo ambalo asilimia 24
ya watu hawana kazi, hii ikiwa ni kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2014.
DW
No comments:
Post a Comment