Monday, October 31, 2016

MKUU WA WILAYA YA KONGWA ATEMBELEA HOSPITALI YA WILAYA NAKUAHIDI GENERATOR NDANI YA WIKI MOJA

Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe Deo Ndejembi Leo ameitembelea Hospitali ya Wilaya ya Kongwa kwa kukaguwa Wodi zote nakusalimia wagonjwa walioko katika wodi hizo, hilo limeambatana na kuzungumza na wagonjwa changamoto wanazokutana nazo nakujua maoni yao zaidi ili kuboresha huduma za Afya.
DC Ndejembi alimalizia kuzungumza na kaimu Mganga mkuu wa Hospitali hiyo Dk. Rehema ambae alizungumzia Changamoto ya Umeme pale Tanesco wanapokata umeme kwani Generator ni mbovu.
DC kamuahidi Mganga Mkuu kuwa Ndani ya Wiki Hii ataipatia Hospitali ya Wilaya ya Kongwa Generator ili Kuondoa Kero hiyo ya Umeme pale umeme wa TANESCO unapokatika.

No comments:

Post a Comment