Tuesday, October 4, 2016

Mkoa wa Singida una Chumvi nyingi ya Asili...!


Leo nimetembelea katika Mbuga ya Mwakilongo ambayo ni maalumu kwa uzalishaji wa Chumvi ya Asili kabisa ni takribani Kilomita 120 kutoka yalipo makao makuu ya Mkoa wa Singida.

Ni katika Kijiji cha Itagata, Kata ya Kikio, Jimbo la Singida Mashariki, Wilaya ya Ikungi.

Kwanza wananchi wa kijiji hiki wamenihakikishia kuwa Hakuna mwananchi anayetumia Chumvi kutoka viwandani yaani Chumvi ya Pakiti badala yake kwa bei Chee wanajipatia Chumvi inayozalishwa katika maeneo yao. Mimi pia nimenunua Debe moja ambalo linauzwa shilingi 5000 tu naamini Mama Leah atalitumia kwa kipindi cha karibu miaka miwili kabisa.

Naaam Nawasalimu sana...!
Mathias Canal (Sauti ya Wanyonge)
0756413465
Itagata-Singida

No comments:

Post a Comment