Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akizungumza na Makundi mbalimbali ya Wakazi wa Dodoma ambao shughulizao
zinahusiana na mazingira kwenye mkutano uliofanyika ukumbi wa Jengo la
Hazina ndogo, Makulu mkoani Dodoma ambapo alisisitiza dhambi ya kuharibu
mazingira haisameheki hivyo kuwataka kila mmoja awe mstari wa mbele
katika kutunza mazingira.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Makundi mbalimbali ya Wakazi wa Dodoma ambao shughulizao zinahusiana na mazingira kwenye mkutano uliofanyika ukumbi
wa Jengo la Hazina ndogo, Makulu mkoani Dodoma.
wa Jengo la Hazina ndogo, Makulu mkoani Dodoma.
Vijana wa DOYODO ni sehemu ya makundi yaliohudhuria mkutano wa Makamu wa Rais mjini Dodoma.
Wazee Mashuhuri wa mji wa Dodoma ni miongoni mwa waliohudhuria mkutano na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Dampo la
kisasa lililopo Chidaye ambalo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
Mhe. Samia Suluhu Hassan alitembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa
dampo hilo.
Kaimu
Mkuu wa Idara ya Mazingira na Taka ngumu wa Manispaa ya Dodoma Bw.
Barnabas Faida (kushoto) akielezea utaratibu utakaotumika wa kutupa taka
katika dampo la kisasa la Chidaye kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye alitembelea na
kujionea maendeleo ya ujenzi wa dampo hilo ambalo linatarajiwa kuanza
kutumia mwezi novemba.
Mhandisi
wa Majengo Bi. Gladness Pesha akimuelezea Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan mgawanyo wa ofisi katika
jengo la Mkuu wa mkoa wa Dodoma.
Jengo la Ofisi ya Mkoa wa Dodoma lililopo eneo la Makulu ambalo lipo kwenye hatua za mwisho za kukamilika.
MAKAMU wa
Rais, Samia Suluhu Hassan, ametaja vigezo vinavyokwamisha Dodoma kuwa
Jiji ikiwa ni pamoja na uharibifu wa mazingira na uzembe wa ukusanyaji
mapato.
Kauli
hiyo aliitoa jana alipokuwa akizungumza na wazee, wafanyabiashara,
vikundi vya usafi wa mazingira na viongozi mbalimbali wa serikali, mjini
hapa.
Alisema
serikali inapohamia Dodoma lazima kuwe Jiji na ili kupata hadhi hiyo
mambo mengi yanahitajika ikiwa ni pamoja na usafi wa mazingira.
Samia
alisema mkoa huo umeathiriwa sana na mabadiliko ya tabia nchi ambayo kwa
asilimia kubwa yamesababishwa na shughuli za kibinadamu kwa kukata miti
ovyo na kuifanya Dodoma kubadilika tofauti na ilivyokuwa awali.
No comments:
Post a Comment