Na Dotto Mwaibale
MAJONZI
na vilio vilitawala ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul
Makonda wakati Kijna Said Mrisho anayedaiwa kujeruhiwa na kutobolewa
macho na Salumu Henjelewe maarufu kama Scorpion Buguruni Sheli alipokuwa
akizungumza na waandishi wa habari mbele ya mkuu wa mkoa Dar es Salaam jana
asubuhi kuwa hata ona tena katika maisha yake kufuatia kujeruhiwa
vibaya kwenye mishipa ya macho na mtuhumiwa huyo na kupoteza uwezekano
wa kuona.
"Nilijua ipo siku moja nitakufa lakini sikutegemea kuwa nitakuja kutolewa macho yangu kikatili kiasi hiki sijui mungu anampango gani na mimi wala sijui nini hatima ya maisha yangu" alisema Mrisho ambapo ukumbi mzima uligubikwa na ukimya sanjari na simanzi huku mke wake Stara Soud akishindwa kujizuia kulia.
"Nilijua ipo siku moja nitakufa lakini sikutegemea kuwa nitakuja kutolewa macho yangu kikatili kiasi hiki sijui mungu anampango gani na mimi wala sijui nini hatima ya maisha yangu" alisema Mrisho ambapo ukumbi mzima uligubikwa na ukimya sanjari na simanzi huku mke wake Stara Soud akishindwa kujizuia kulia.
Mrisho
alisema anamshukuru sana Rais John Magufuli na Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam, Paul Makonda kwa jitihada walizofanya za kumsaidia kupata
matibabu lakini imeshindikana kwa kuwa mishipa yote yenye uwezo wa
kumfanya aweze kuona imeharibiwa vibaya na mtuhumiwa huyo hivyo hataweza
kuona tena katika maisha yake.
"Kama
mishipa isingeharibiwa kwa visu mama yangu kipenzi Halima Lwiza
Abdallah alikuwa yupo tayari kutoa jicho lake moja kwa ajili ya
kunisaidia niweze kuona lakini kwa bahati mbaya hilo halitawezekana
baada ya madaktari kunieleza kuwa mishipa ya macho yangu imeharibiwa" alisema Mrisho kwa huzuni na kuanza kulia.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alisema
wamepokea kwa huzuni taarifa hiyo ya madaktari na kumuomba Mrisho
asikate tamaa kwani serikali itaangalia jinsi ya kumsaidia.
Makonda
alisema serikali itatoa sh.milioni 10 kama mtaji ili ziweze kumsaidia
wakati wakiangalia namna ya kuwashirikisha watu wengine kwa ajili ya
kumsaidia.
Makonda
alisema serikali itamsaidia kufanyiwa upasuaji wa kuwekewa macho ya
bandia ili awe katika mwonekano wa kawaida ingawa atakuwa haoni.
"Pamoja
na kumpatia kiasi hicho cha fedha katika kipindi hiki cha mpito ambacho
atakuwa akihitaji kwenda katika matibabu na sehemu zingine tutakuwa
tukimsaidia usafari wa kwenda maeneo hayo" alisema Makonda.
Kijana
Said Mrisho anayedaiwa kujeruhiwa na kutobolewa macho na Salumu
Henjelewe maarufu kama Scorpion (kulia), akilia kwa uchungu wakati
akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari mbele ya Mkuu wa Mkoa
wa Dar es Salaam, Paul Makonda jana. Kushoto ni mke wake, Stara Soud
No comments:
Post a Comment