Jeshi
la Polisi Mkoani Rukwa linamshikilia Diwani wa kata ya Izira, Paschael
Silimba (Chadema) baada ya kumkamata akiwa na dawa za kulevya aina ya
bangi na bunduki moja aina ya gobole.
Kamanda
wa Polisi wa mkoa huo, Kamishna Msaidizi wa Polisi, George Kyando
amesema kuwa jeshi hilo lilimkamata Kyando katika eneo la soko kuu
ambalo hufanyia biashara yake ya kuuza mifuko ya salfeti, baada ya
kupata taarifa na kuamua kumfuatilia.
Alisema
kuwa baada ya kumpekua katika vifurushi vya bidhaa hiyo anayoiuza kwa
kushirikiana na mkewe, walibaini uwepo wa bangi kiasi cha robo kilo.
“Baada
ya kufanya upekuzi kwenye duka la diwani huyo, tumefanikiwa kukamata
bangi kiasi cha robo kilo. Ni bangi kavu ambayo imeshaandaliwa tayari
kwa ajili ya kufanya packing na kuuzwa,” alisema Kamanda Kyando.
Akizungumzia
silaha aina ya gobole waliyoikuta nyumbani kwa diwani huyo anayodaiwa
kuimiliki kinyume cha sheria, alisema ingawa ni silaha ya kizamani ina
nguvu ya kuua tembo.
“Silaha
hii ina nguvu sana, ina uwezo wa kuua tembo na ni hatari sana akipigwa
binadamu kwa silaha hii. Kwahiyo msiione hapa mkaidharau, ina nguvu
sana,” aliongeza.
Kamanda
Kyando aliwataka viongozi wote waliopewa dhamana na wananchi kutotumia
nyadhifa zao kufanya uhalifu. Alitoa wito wito kwa wananchi kuendelea
kushirikiana na jeshi hilo kufichua uhalifu bila kujali waliofanya
uhalifu huo.
No comments:
Post a Comment