Tangu
mkazi mmoja wa Dar es Salaam Said Ally alivyoeleza namna alivyofanyiwa
ukatili na kutobolewa macho yake mawili mbele ya umati wa watu katika
eneo la Buguruni, watu wengi wamejitolea kwa hali na mali kumsaidia ili
aweze kumudu gharama za maisha.
Said
Ally ambaye alieleza stori yake kupitia kipindi cha Leo Tena cha Clouds
Fm, watu wameweza kumchangia fedha, vitu vyakumsaidia kuendesha maisha
yake na vitakavyomuingizia kipato kwa sababu hawezi tena kufanya kazi
kutokana na kupoteza uwezo wa kuona baada ya kutobolewa macho.
Miongoni
mwa misaada aliyoipokea hadi sasa ni pamoja na TZS milioni 10 ambazo
amepewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ambaye amesema
kuwa yupo kwa ajili ya kuwasaidia wanyonge na wenye mahitaji kama
alivyoagizwa na Rais Magufuli, lakini pia Makonda ameahidi kumlipia
gharama aweze kufundishwa kusoma kwa kutumia alama na pia kumnunulia
fimbo maalum ya kumsaidia kutembelea.
Mbali
na Mkuu wa Mkoa, Said amepewa msaada wa pikipiki 5 ambapo kati ya hizo,
pikipiki 2 ni msaada Infotech na pikipiki 3 ni msaada kutoka TSN. Pia
Adamjee amemsaidia Said Bajaji mbili ambapo vyote hivi vitaweza
kumsaidia kuingiza kipato na kuendesha maisha yake. Vitu vyote hivi
vimepatikana kutokana na jitihada zilizofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Dar wa
kutafuta watu wa kumsaidia Said.
Kwa
upande mwingine GSM kupitia ushawishi wa Mkuu wa Mkoa imesema kuwa
itamsaidia Said Ally nyumba ya kuishi na yeye mwenyewe alishukuru sana
na kusema kuwa angependa nyumba hiyo iwepo maeneo ya Tabata, Dar es
Salaam kwani ndilo eneo alilolizoea kwani amekua akiishi hapo tangu
mwaka 1999.
Kwa
upande mwingine, mwanamuziki Diamond Platnumz amejitolea msaada wa TZS
milioni 2. Wakati Said akifanya mahojiano jana na Clouds Fm alisema kuwa
moja ya vitu alivyo-miss kuvitazama ni pamoja na video ya Salome ya
Diamond Platnumz, kitu kilichomsukuma mwanamuziki huyo kufika Clouds Fm
na kutoa msaada.
Said
Ally ambaye ni baba wa familia ya watoto 5, kabla ya kukumbwa na mkasa
huo wa kuharibiwa macho yake na mtuhumiwa Scorpion alikuwa akifanya kazi
ya kinyozi Tabata.
Mtuhumiwa
aliyehusika na tukio hili tayari anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa
uchunguzi kuweza kufanyika ili afikishwe mahakamani na haki iweze
kupatikana.
No comments:
Post a Comment