Friday, October 14, 2016

DC NDEJEMBI AFANYA MDAHALO KUMUENZI BABA WA TAIFA


Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mh Deo Ndejembi Leo Amemuenzi Baba wa Taifa kwa kutoa somo Kwa vijana nchini kumuenzi baba wa Taifa Kwa vitendo.

Ameyasema hayo kufuatia mjadala mzito wa kujadili mada katika Mdahalo wa kumuenzi mwalimu Nyerere Kwa vitendo katika maisha Yao ya kila siku.
Mkuu wa Wilaya kawaeleza Wananchi kuwa Nilazima Wazingatie nakuimaliza Rushwa, Wawe Wazalendo, na wanapaswa wawe Waadilifu kwani Ndio Haswaa Misingi aliyotuachia Mwalimu Nyerere. DC Kayasema hayo baada ya vijana wengi kusema hawamuenzi mwalimu kwa Vitendo.

Mdahalo huo umewakutanisha watumishi wa Hamshauri ya Kongwa, Walimu na wanafunzi pia wadau wa maendeleo wa Wilaya ya Kongwa ikiwa Kama kielelezo cha siku ya kifo ya Mwalimu Nyerere ambapo kiwilaya imefanyika katika ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa.
Mada Kuu ilikuwa ikisema

"JE! VIJANA WANAMUENZI BABA WA TAIFA KWA VITENDO?"

Kabla ya Mjadala huo Ilifanyika Dua Maalumu yakumuombea Baba wa Taifa nakuliombea Taifa kwa Ujumla ili Taifa liishi Misingi ya Mwalimu.

No comments:

Post a Comment