Mbunge wa
jimbo la Nzega Mjini Mhe, Hussein Bashe (kushoto) akiongea na
Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Bwana Sunil Colaso (kulia) wakati
alipotembelea ofisi za Airtel juu ya program ya WanaNzengo Airtel FURSA
inayowawezesha vijana wajasiriamali waishio katika kata 10 zilizoko
ndani ya Jimbo la Nzega Mjini mkoani Tabora kupata mikopo yenye riba
nafuu itakayosaidia kutatua changamoto za ajira kwa vijana. Programu hii
inaendeshwa kwa ushirika kati ya Airtel Tanzania kupitia mpango wake wa
Airtel FURSA “Tunakuwezesha” na asasi iliyoundwa kimikakati na Mbunge
huyo ya Nzega Urban Trust Fund ili kumaliza tatizo la umasikini wa
kipato katika jimbo la Nzega Mjini.
Mkurugenzi
Mkuu wa Airtel Bwana Sunil Colaso (kulia) akzungumza na Mbunge wa jimbo
la Nzega Mjini Mhe, Hussein Bashe (kushoto)wakati alipotembelea ofisi
za Airtel juu ya program ya WanaNzengo Airtel FURSA inayowawezesha
vijana wajasiriamali waishio katika kata 10 zilizoko ndani ya Jimbo la
Nzega Mjini mkoani Tabora kupata mikopo yenye riba nafuu itakayosaidia
kutatua changamoto za ajira kwa vijana. Programu hii inaendeshwa kwa
ushirika kati ya Airtel Tanzania kupitia mpango wake wa Airtel FURSA
“Tunakuwezesha” na asasi iliyoundwa kimikakati na Mbunge huyo ya Nzega
Urban Trust Fund ili kumaliza tatizo la umasikini wa kipato katika jimbo
la Nzega Mjini.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso (kushoto), akikabidhi hundi
ya kiasi cha shilingi Milioni 20, kwa Mbunge wa jimbo la Nzega Mjini
Mhe, Hussein Bashe (kulia) Kwa ajili ya kuwezesha vijana wajasiriamali
waishio katika kata 10 zilizoko ndani ya Jimbo la Nzega Mjini mkoani
Tabora kupata mikopo yenye riba nafuu itakayosaidia kutatua changamoto
za ajira kwa vijana. Programu hii inaendeshwa kwa ushirika kati ya
Airtel Tanzania kupitia mpango wake wa Airtel FURSA “Tunakuwezesha” na
asasi iliyoundwa kimikakati na Mbunge huyo ya Nzega Urban Trust Fund ili
kumaliza tatizo la umasikini wa kipato katika jimbo la Nzega Mjini.
Kampuni
ya simu za mkononi ya Airtel kupitia mfuko wake maalum wa kusaidia jamii
wa Airtel FURSA Tunakuwezesha leo imekabidhi hundi ya shilingi milioni
20 kwa Mbunge wa Nzega ikiwa ni harakari za kukamilisha dhamira yake ya
kushirikiana na jamii katika kuinua vijana sehemu mbalimbali hapa
nchini.
Akikabidhi
hundi hiyo Mkurugenzi mkuu wa Airtel Bw Sunil Colasa alisema “Airtel
imejipanga kwa kuhakikisha vijana wanaendelea kunufaika na mradi wa
Airtel FURSA kwa kuwapatia misaada ya kukamilisha mipango yao
waliyoipanga kwa kupunguza changamoto walizonazo ikiwemo ya ukosefu wa
ajira na mtaji ili watimize malengo yao katika biashara”
“Tunaamini
kupitia ushirika wetu na Mbuge Nzega Mh, Hussen Bashe mfuko wa Nzega
Trust Fund utasaidia wananchi ndani ya vijiji 21 katika jimbo hilo
ambapo malengo yetu ni kufanya mradi huu kuwa endelevu hata kwa majimbo
mengine nchini” alisema Bw, Colasa
kwa
upande wake Mbunge wa Nzega Mjini Mh, Hussen Bashe aliishukuru Airtel
nakuahidi kusimamia mradi huo wa ukopeshaji kwa ajili ya kuweza kuinua
vipato vya wananchi wa Nzega kama ilivyokusudiwa
“Nitoa
wito kwa wananchi wote wenye malengo ya kujiendeleza kujitoza na
kujisajili katia Mfuko wetu wa Nzega Trust Fund niliouanzisha kwaajili
ya kuhakikisha tunaungana na wadau wenye nia ya kusaidia jamii kama
Airtel FURSA ili kupunguza changamoto za maendeleo kwa wananchni hasa
kwa wanaokosa mitaji ya kuendesha Miradi yao mbalimbali”
“Airtel
tayari wamezikabidhi pesa hizi kwangu ambazo tutazikopesha kwenu kwa
Riba ya 1.5% pale unaporejesha na faida inayopatikana bado itaendelea
kuwasaidia vijana wengine watakaotaka kukopa” Alieleza Mh Bashe
Mradi wa
Airtel Fursa umeanzishwa Mei mwaka uliopita na tayari umewafikia vijana
zaidi ya Elfu tano kutoka katika mikoa kumi nchini ikiwa ni pamoja na
vijana zaidi ya 100 waliowezeshwa kwa kupewa mitaji na vitendea kazi
mbalimbali
No comments:
Post a Comment