Sunday, September 11, 2016

WAZIRI MKUU AONGOZA WANANCHI KUAGA MIILI YA WALIOKUFA KWA TETEMEKO BUKOBA

buko1
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapa  pole baadhi ya majeruhi wa  tetemeko la ardhi lililotokea  mkoani Kagera  wakati alipotembelea hospitali ya mkoa wa Kagera mjini  Bukoba  Septemba 11, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
buko2

buko3
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapa  pole baadhi ya majeruhi wa  tetemeko la ardhi lililotokea  mkoani Kagera  wakati alipotembelea hospitali ya mkoa wa Kagera mjini  Bukoba  Septemba 11, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
buko4
Waziri  Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapa pole  wafiwa  wakati alipokwenda mjini Bukoba Septemba 11, 2016 kukagua athari za tetemeko la ardhi na kuwafariji majeruhi, wafiwa na wananchi wa mkoa wa Kagera. Alikuwa katika Ibada ya kuwambea marehemu hao kwenye uwanja wa Kaitaba .(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
buko5
Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa akitoa heshima za mwisho kwa marehemu walipoteza maisha kutokana na tetemeko la ardhi  mkoani kagera katika ibad maalum ya kuwaombea marehemu hao iliyofanyika kwenye uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba Septemba 11, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
buko6
buko7
buko8
buko9
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama nyufa zililizosababishwa na tetemeko la ardhi mkoani Kagera wakati alipotembelea Shule ya Sekondari ya Nyakato kuona athari za tetmeko hilo Septemba 11, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
buko10
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama nyufa zililizosababishwa na tetemeko la ardhi mkoani Kagera wakati alipotembelea Shule ya Sekondari ya Nyakato kuona athari za tetmeko hilo Septemba 11, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
buko11
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananfunzi wa Shule ya Sekondari ya Nyakato mkoani Kagera wakati alipokwenda  shuleni hapo Septemba 11, 2016 kujionea athari za tetemeko la ardhi lililoukumba mkoa huo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
buko12
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipita mbele ya bweni la shule ya sekondari ya Ihungo  mkoani Kagera  ambalo liliporomoka kutokana na tetemeko la ardhi lililoukumba mkoa huo .  Alikuwa katika  ziara ya kukagua  athari za tetemeko hilo na kuwapa pole wananchi, Septemba 11, 2016.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
buko13
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameongoza maelfu ya wananchi wa Manispaa ya Bukoba mjini kuaaga miili ya watu 16 waliofariki kutokana na tetemeko la ardhi lililotokea jana (Jumamosi, 10 Septemba, 2016 mkoani Kagera.

Tetemeko hilo lilitokea jana Alasiri limesababisha vifo vya watu 16 na wengine 253 kujeruhiwa. Pia limesababisha maelfu ya wananchi kukosa makazi baada ya nyumba 840 kuanguka na nyingine 1264 zikipata nyufa yakiwemo majengo 44 ya taasisi mbalimbali za umma.

Kufuatia tukio hilo Waziri Mkuu ambaye alimuwakilisha Mheshimiwa Rais, Dk. John Magufuli amewaomba wananchi kuwa watulivu wakati Serikali ikiendelea kufanya tathmini ya athari zilizotokana na maafa hayo.

“Poleni sana tukio hili ni kubwa na halijawahi kutokea nchini. Haya yote ni mapenzi ya Mwenyezi Mungu. Tuendelee kuwa na imani na watulivu  Serikali ipo pamoja nanyi na haitawatupa mkono,” amesema.

Waziri Mkuu amesema Kamati ya Maafa ambayo ipo katika Ofisi ya Waziri ya Mkuu itakwenda wilaya za Kyerwa, Karagwe na Bukoba mjini kwa ajili ya kufanya tathmini na kubaini athari zilizosababishwa na tetemeko hilo na kuona namna ya kuwasaidia waathirika.

Wakati huo huo Waziri Mkuu amewaagiza viongozi wa mkoa huo kuchukua hatua za haraka kwa kuwatafutia eneo salama la kulala wanafunzi wa Shule ya Sekondari Nyakato ambayo mabweni yake yote yameathirika na tetemeko hilo na hayafai kutumika.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo baada ya kutembelea shule hiyo na kujionea namna mabweni ya shule hiyo yalivyopata nyufa hali iliyosababisha wanafunzi kulala uwanjani.

Pia Waziri Mkuu ameiagiza Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kuangalia kama kuna tetemeko linguine linaweza kutokea nchini ili Serikali iweze kuchukua tahadhari pamoja na kutoa elimu kwa umma namna ya kujikinga.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali Mstaafu, Salum Kijuu amesema kwa sasa wanaendelea na jukumu la kuwatafutia makazi wananchi ambao nyumba zao zimeanguka. Pia mkoa unaendelea kufanya tathmini ya kina kujua athari zilizosababishwa na tetemeko hilo.

Awali Waziri Mkuu alitembelea Hospitali ya Mkoa wa Kagera ambako majeruhi 170 wamelazwa na kutoa pole na kwamba anawaombea kwa Mwenyezi Mungu wapone haraka na wenye matatizo ambayo yanahitaji matibabu kwenye hoispitali kubwa Serikali itahakikisha wanapelekwa huko na kuhudumiwa.

No comments:

Post a Comment