Mbunge wa
Jimbo la Pangani Mhe. Jumaa Awesu akizungumza na wananchi wa Jimbo hilo
katika uzinduzi wa Kivuko cha Mv. Tanga na Gati ya bandari ya Pangani
uliofanyika Mkoani Tanga.
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) Eng.Karim Mattaka
akisoma taarifa ya ujenzi wa Gati ya bandari ya Pangani kwa Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (hayupo pichani)
katika uzinduzi wa Kivuko cha Mv. Tanga na Gati hiyo uliofanyika Mkoani
Tanga.
Mkuu wa
Mkoa wa Tanga Ndg. Martin Shigela akielezea taarifa ya utekelezaji wa
Miradi ya Miundombinu katika Mkoa wa Tanga kwa Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (hayupo pichani) katika
uzinduzi wa Kivuko cha Mv. Tanga na Gati hiyo uliofanyika Mkoani Tanga.
Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akifafanua jambo
kwa wananchi wa Pangani katika uzinduzi wa Kivuko cha Mv. Tanga na Gati
hiyo uliofanyika Mkoani Tanga.
Wananchi
wa Pangani wakishangilia ujio wa Kivuko kipya cha Mv. Tanga Wilayani
hapo kinachotoa huduma ya usafirishaji kati ya Pangani na Bweni.
Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa pamoja na
watendaji wa Serikali na Wizara wakikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi
wa Kivuko cha Mv. Tanga kulia ni Mkuu wa wilaya ya Pamgani Mhe. Zainabu
Abdallah Issa .
Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa pamoja na
watendaji wa Serikali na Wizara wakizindua Gati la Bandari ya
Tanga.Ukamilifu wa Gati hiyo utasaidia Meli mbalimbali kuweza kutia
nanga wilayani Pangani.
Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa pili kulia)
akisafiri na wakazi katika Kivuko cha Mv.Tanga kutoka Pangani kwenda
Bweni mara baada ya uzinduzi. Wanne kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara
hiyo (Sekta ya Ujenzi) Eng. Joseph Nyamhanga.
Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amezindua kivuko
kipya na cha kisasa cha Mv. Tanga kinachotoa huduma ya usafirishaji
kati ya Pangani na Bweni na kuzindua Gati ya Bandari ya Pangani wilayani
pangani mkoani Tanga.
Akizungumza
katika uzinduzi huo Waziri Mbarawa amesema kuwa ujio wa kivuko hicho
utafungua fursa za kibiashara na kuchochea maendeleo ya kiuchumi
wilayani hapo.
“Naamini
ujio wa kivuko hiki utarahisisha huduma za kijamii na maendeleo ya
kiuchumi wilayani hapa, hivyo naomba mkitunze vizuri kivuko hiki ili
kiweze kudumu kwa muda mrefu”, amesema Prof.Mbarawa.50 242
Ameongeza
kuwa katika kuhakikisha huduma za kivuko zinakuwepo muda wote wilayani
hapo, Serikali kupitia Wizara hiyo imetenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa
boti ambayo itatumika kama mbadala wa usafiri wakati wa usiku katika
maeneo hayo ambapo kivuko cha Mv.Tanga hakifanyi kazi.
Kuhusu
ujenzi wa Gati ya bandari ya Pangani Waziri Mbarawa ameseama kuwa ujenzi
wa gati hiyo utapelekea Meli kubwa kuweza kutia nanga na kurahisisha
usafiri wa moja kwa moja kutoka Pangani kwenda visiwa vya Unguja na
Pemba.
Amefafanua
kuwa Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wataanzisha huduma
ya boti za haraka kutoka Pangani kwenda Mkokotoni Zanzibar hivyo
kufungua fursa za kibiashara na kitalii baina ya Tanga na Zanzibar.
Kwa
upande wa huduma za mawasiliano ya simu wilayani hapo, Prof.Mbarawa
amesema kuwa huduma hiyo itaanza mwezi Desemba mwaka huu kwa mkandarasi
kufika na kuanza ujenzi wa miundombinu ya simu na hivyo kuondoa tatizo
la mawasiliano wilayani hapo.
Katika
hatua nyingine Prof. Mbarawa amehahidi kuanza ujenzi wa Barabara ya
Tanga-Pangani-Saadani hadi Bagamoyo (KM 242) kwa kiwango cha lami
ifikapo mwakani.
Amefafanua
kuwa ujenzi wa barabara hiyo utakuwa wa awamu ili kuweza kuharakisha
kukamilika kwake ambapo awamu ya kwanza itahusisha kipande cha barabara
ya Tanga- Pangani (KM 50) na kuongeza kuwa ujenzi wa barabara hiyo
utafungua fursa za kiuchumi kati ya Tanga na Pangani.
“Naahidi
kujenga barabara hii ambayo ni kiungo kati ya Tanga na Pangani, naamini
ukamilifu wake utalete maendeleo mkoani hapa”. Amesisitiza Prof.
Mbarawa.
Kwa
upande wake Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Eng.Joseph Nyamhanga amezipongeza
kampuni za Songoro Marine na Alpha Logistic kwa kumaliza kwa wakati
ujenzi wa kivuko na Gati ya bandari hiyo.
Naye
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Eng.Manase
Ole-kujan amesema kuwa kivuko cha Mv.Tanga kimejengwa kwa sh.bilioni nne
ambapo kina uwezo wa kubeba tani 50 abiria 100 na magari madogo 6 kwa
wakati mmoja.
Ujenzi wa
Kivuko cha Mv. Tanga ni moja ya utekelezaji wa ahadi ya Mhe.Rais
Dkt.John Pombe Magufuli aliyoitoa wakati wa kampeni ya uchaguzi mkuu wa
mwaka 2015 wilayani Pangani Mkoani Tanga.
No comments:
Post a Comment