Ibada ya
Hijja ya kila mwaka inayotekelezwa na Waislamu imeanza Jumamosi
(10.09.2016) nchini Saudi Arabia huku hatua kali za kiusalama zikiwa
zimeimarishwa kwa takriban mahujaji milioni 1.5 wanaoshiriki hija hiyo.
Ibada ya
Hijja ya kila mwaka inayotekelezwa na Waislamu imeanza Jumamosi
(10.09.2016) nchini Saudi Arabia huku hatua kali za kiusalama zikiwa
zimeimarishwa kwa takriban mahujaji milioni 1.5 wanaoshiriki hija hiyo.
Baada ya
kufanyika kwa taratibu za awali za ibada hiyo katika Msikiti Mkuu katika
mji wa Mecca eneo takatifu kabisa kwa Waislamu duniani mahujaji hao
Jumamosi wameanza kuelekea eneo la tambarare la Mina lilioko kama
kilomita tano mashariki ya Meccca kwa kutumia vyombo mbali mbali vya
usafiri na hata kwa miguu chini ya hali ya joto inayopindukia nyuzi joto
40.
Mahujaji
hao watakuwa wanafuata nyayo za Mtume Muhammad (SAW) aliyefanya
utaratibu huo huo wa ibada miaka 1,400 iliopita.Mamia kwa maelfu ya
mahujaji wakiwa katika mavazi yao meupe yasiokuwa na mishono walianza
kuondoka mji mtakatifu wa Mecca Jumamosi alfajiri kwa safari yao hiyo ya
Mina ambapo watalala huko na watakamilisha hijja kwa kwenda kusimama
kwenye mlima Arafat hapo Jumapili.
Tarehe 24
Septemba mwaka jana Mina palikuwa ndio mahala kulikotokea maafa mabaya
kabisa katika historia ya hija kutokana na mkanyagano wakati mahujaji
walipokuwa wakielekea kwenye Daraja la Jabarat kwa ajili ya kumpiga mawe
shetani. Mwaka huu kumpiga mawe shetani kutaanza Jumatatu.
Usalama waimarishwa
Juu ya
kwamba serikali ya Saudi Arabia imeendelea kusisitiza kwamba idadi ya
watu waliokufa katika mkanyagano huo walikuwa 769 data kutoka maafisa wa
nchi za kigeni kutoka zaidi ya nchi 30 wametowa idadi mara tatu zaidi
ya hiyo kwamba waliokufa ni 2,297.
Saudi
Arabia ilitangaza uchunguzi wa makanyagano huo lakini matokeo katu
hayakuwahi kutangazwa.Safari hii hatua kadhaa za kuimarisha usalama
zimechukuliwa ikiwa ni pamoja na mahujaji kuvalishwa vibangili vya
elektroniki vitakavyowasaidia kuwatambulisha wakati wa
msongamano.Vibangili hivyo vitahifadhi data zao binafsi baada ya maafisa
wa nchi za kigeni kuelezea wasi wasi wao juu ugumu wa kuwatambuwa
mahujaji waliokufa kutokana na mkanyagano.Hatua hizo za usalama
zinajumuisha pia uwekaji wa mamia ya kamera za uchunguzi katika maeneo
takatifu.
Maelfu ya
wananchi wa Iran hawakuweza kuhudhuria hijja ya mwaka huu kutokana na
mvutano wa mrefu kati ya mataifa hayo ambapo Iran ina waumini wengi wa
madhehebu ya Shia na Saudi Arabia linalodhibitiwa na Waislamu wa madhebu
ya Sunni ambao ndio walio wengi nchini humo na mvutano wao ulizidi
kupaliliwa kutokana na mkanyagano wa mwaka jana.
Wairan wakosa hijja
Licha ya
hatua ambazo Saudi Arabia inasema imezichukuwa ili kuzuwiya msongamano
na kuboresha usalama, serikali ya Iran inaendelea kuhoji haki ya utawala
wa kifalme wa nchi hiyo kusimamia maeneo hayo takatifu kabisa kwa
Waislamu.Nchi hizo hazina uhusiano wa kibalozi na zinahitilafiana juu ya
masuala kadhaa ya kanda vikiwemo vita vya Yemen na Syria .
Iran ndio
iliopoteza mahujaji wengi katika mkanyagano wa mwaka jana ambao
wanatajwa kufikia 464 na kwa mara ya kwanza haiukutuma mahujaji wake
mwaka huu baada ya miongo mingi baada ya nchi hizo kushindwa kukubaliana
juu ya masuala ya usalama na vifaa.Maelfu ya watu nchini Iran hapo
Ijumaa waliandamana kupinga kutokuwepo kwa nchi yao katika ibaada hii ya
hijja.
Takriban
Waislamu milioni 1.3 kutoka takriban nchi 160 wako nchini Saudi Arabia
mahala ulikozaliwa Uislamu kwa ajili ya ibada ya hijja ya mwaka huu
ikiwa ni ziada ya mahujaji wa ndani ya nchi 102,000.
DW
No comments:
Post a Comment