Tuesday, September 13, 2016

Vikosi vya UN vyaridhishwa na hali ya mambo Syria

Staffan De Mistura amesema kuwa anatarajia usambazaji wa misaada kuanza hivi karibuni
Staffan De Mistura amesema kuwa anatarajia usambazaji wa misaada kuanza hivi karibuni
Vikosi maalum vya umoja wa mataifa nchini Syria vimesema vimeridhishwa na kupungua kwa mapigano tangu usitishwaji wa mapigano kuanza siku ya jumatatu.

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa Staffan De Mistura amesema kuwa anatarajia usambazaji wa misaada kuanza hivi karibuni,
Vikosi maalum huko Syria vimesema kuwa kuna utulivu maeneo mengi ya nchi
Vikosi maalum huko Syria vimesema kuwa kuna utulivu maeneo mengi ya nchi
Amesema pia kipaumbele cha sasa ni kuandaa usambazaji wa misaada katika maeneo yaliyoshikiliwa na waasi huko Aleppo.

Mistura ameonya kuwa usitishwaji wa mapigano unaweza kuhatarishwa na athari za matukio ya vurugu yanayohusisha pande zenye mzozo.
Kwa mara ya kwanza imeripotiwa kutokuwepo kwa mauaji ya raia
Kwa mara ya kwanza imeripotiwa kutokuwepo kwa mauaji ya raia
Wizara ya mambo ya nje ya Syria imeonya kuwa vifaa havitaruhusiwa kuingia Aleppo bila ruhusa yake.

Kusitishwa kwa mapigano kumeleta utulivu katika maeneo ya wakazi yanayoshikiliwa na waasi mjini Aleppo huku watoto wakicheza nje kwa mara ya kwanza bila kuwepo kwa ndege za mashambulizi, lakini Urusi imeshutumu waasi kwa ukiukaji zaidi ya mara ishirini nchi nzima wa makubaliano ya kusitisha mapigano na kuitaka Marekani kuweka nguvu kwa kundi wanalounga mkono.

Vikosi maalum huko Syria vimesema kuwa kuna utulivu maeneo mengi ya nchi tangu kuanza kwa usitishwaji wa mapigano wa muda siku ya jumatatu.

Mkuu wa shirika la misaada la Islamic Relief huko Syria, Ahmed Mohamoud ameiambia BBC kuwa kuwa shirika lake litafanya kila liwezakano lakini ana mashaka juu ya usitishwaji wa mapigano kuendelea.

"Ukilinganisha na siku zilizopita, hakuna shaka vurugu zimepungua. Ukizingatia ni masaa 24, kwa masaa 48 ya usitishwaji yatakua muhimu sana kwasababu hiyo ni tathmini kwa pande zote mbili kuhusu kiwango cha kupungua kwa uhasama kwa jinsi walivyokubaliana siku ya ijumaa usiku" Staffan De Mistura, Mjumbe wa umoja wa mataifa Syria  
BBC

No comments:

Post a Comment