Mkurugenzi
mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Ileje Haji Mnasi akiwa katika
makumbusho ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyererealipotembele
hivi karibu na kujifunza mambo mbalimbali aliyowahi kuyafanya hayati
baba wa taifa kwa ajili ya kuleta maendeleo ya nchi nzima

Mkurugenzi
mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Ileje Haji Mnasi akiwa katika
kaburi la marehem Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere

Na Fredy Mgunda,Musoma.
VIONGOZI wa vyama vya Siasa wametakiwa kuiga kwa vitendo uzalendo na moyo wa kujitoa aliokuwa nao
Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere enzi za uhai wake ili kuliwezesha Taifa kupiga hatua kimaendeleo
Kauli
hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Ileje Bw. Haji
Mnasi ambaye kitaaluma ni mwalimu mara baada kutembelea Kaburi na
Makumbusho ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere eneo la Mwitongo wilayani Butiama.
“mimi
kitaaluma ni mwalimu hivyo namuezi mwalimu kwa vitendo hata nilipokuwa
afisa elimu iringa nilikuwa naingia darasani kufundi na sasa
nitahakikisha nazilinda mali za taifa,nasisitiza
uwajibika,uzalendo,uandilifu na nidhamu katika kulitumikia taifa
laTanzania kama unakumbuka mwalimu alikuwa anapenda kutumia neno (it can
be done play your part) kila mtu atimizi majukumu yake” Amesema Mnasi.
Amesema
kuwa kumbukumbu za Baba wa Taifa zilizohifadhiwa vizuri katika
makumbusho hiyo zina mambo mengi ya kujifunza ambayo wanasiasa
wanatakiwa kuyafanya kwa vitendo hasa uzalendo kwa nchi, uvumilivu,
upendo na moyo wa kujitoa kwa dhati kuwatumikia wananchi.
“Kupitia
kumbukumbu hizi sisi watumishi tumejifunza ukomavu wa demokrasia
aliokuwa nao Mwalimu Nyerere akiwa ndani na nje ya Bara la Afrika,
wengi wanadhani Demokrasia ni wakati wa uchaguzi tu, kumbe demokrasia ni
pamoja na kuheshimu watu wengine” Amesema Mnasi.
Ameeleza kuwa maisha aliyoishi Baba wa Taifa ni mfano wa kuigwa na viongozi na watanzania wote hasa pale alipojitofautisha na viongozi wengi wa Bara la Afrika alipoepuka tamaa ya madaraka na mali kwa manufaa ya taifa.
“Sote ni
mashahidi kupitia kumbukumbu zake tumeona mahali alipokuwa anaishi
mwalimu kabla hajajengewa nyumba na Jeshi kama Rais mstaafu wengi
walitegemea asingeishi katika eneo lile, kumbukumbu hii nzuri
aliyoiacha inatufundisha watanzania kuwa mwalimu aliitanguliza Tanzania
mbele kuliko maslahi yake binafsi” Amesisitiza Mnasi.
Bw. Mnasi
amebainisha kuwa serikali itaendelea kumuemzi Baba wa Taifa kwa yale
aliyoyafanya na kuyasimamia kwa manufaa ya taifa huku akitoa wito kwa
viongozi wa vyama vya Siasa wawe na kiasi na waridhike na vile walivyonavyo.
“Suala la
kuridhika na kuwa na kiasi linapaswa kuzingatiwa, wanasiasa wanapaswa
kuwaheshimu wananchiwanaowachagua kupitia chaguzi mbalimbali, matokeo
yanapotoka kama ni sahihi basi wanasiasa wakubaliane na maamuzi yao”
Ameainisha Mnasi.Bw. Mnasi amemalizia kwa kuwataka watendaji wote wa
serikali ya wilaya ya Ileje kufanya kazi kwa
uaminifu,uadilifu,kuwajibika kwenye majukumu yao na kujituma na kamwe
hata kuwa tayari kuwavumilia watendaji ambao ni wazembe kazini.
Kwa
upande wake Mhifadhi wa Makumbusho ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius
Kambarage Nyerere Bw. Jacob Thomas amesema kuwa watanzania wanayo mengi
ya kujifunza kupitia vitu alivyoviacha Baba wa Taifa ambavyo
vimehifadhiwa katika Makumbusho hiyo.
Amesema
kuwa maisha ya uadilifu aliyoishi enzi za uhai wake na mchango wake
katika kuiletea maendeleo Tanzania na Bara la Afrika vinapaswa kuenziwa
kwa nguvu zote na viongozi wa Tanzania.
No comments:
Post a Comment