
Ndugu zangu, Januari 17, 2014 nilisikia hayo. Soma hapa.. Bwana Shamba Kilasi ananiambia; " Mwenyekiti, Tandahimba ni Wilaya tajiri kuliko zote Mtwara!"
Kwamba inacheza ' Ligi moja ya kiuchumi' na Ilala na Kahama. Naambiwa mwaka 2013 wakulima wa korosho wa Tandahimba walivuna tani takribani 46 elfu na kilo moja ya korosho wameuza kwa shilingi 1, 200//=. Hivyo, wakulima hao walijipatia shilingi zipatazo bilioni 59.
Nikamwuliza bwana shamba Kilasi; " Mbona utajiri huo wa Tandahimba hauonekani katika huduma na miundo mbinu ya Tandahimba. Maana, kutoka Mtwara tu kwenda Tandahimba ni shughuli inayokuhitaji ubebe korosho za kutafuna njiani.
Maggid,
No comments:
Post a Comment