Leo napenda ufahamu kuwa endapo utapata nafasi ya kula angalau chungwa
moja tu kila siku basi tambua wazi kuwa kuna hizi faida hapa chini
utakuwa unazzipata kila unapotumia tunda hilo.
Kwanza utauhakikishia mwili wako usalama mkubwa zaidi wa kiafya kutokana
na tunda hilo kuwa na kiwango cha kutosha cha vitamin C ambayo husaidia
kuimarisha kinga za mwili na kumfanya mhusiaka kutosongwa na magonjwa
ya mara kwa mara kirahisi.Lakini pia ulaji wa chungwa mara kwa mara utaupatia mwili wako madini ya
potassium, calcium, folate, pamoja na vitamin B ambavyo vyote kwa
pamoja ni muhimu ndani ya miili yetu wanadamu.
Pamoja na hayo, chungwa pia lina nyuzinyuzi 'fiber' ambazo huhitajika
sana katika kufanya zoezi la umeng'enyaji chakula ndani ya tumbo na
hivyo kumsaidia mhusika kuepukana na matatizo mbalimbali ikiwa ni pamoja
na ukosefu wa choo.
No comments:
Post a Comment