Maandamano yaliyopangwa na serikali katika mji wa Bujumbura dhidi ya Ufaransa na azimio la Umoja wa Mataifa Julai 30, 2016.
Warundi
wasiozidi kumi na tano wameandamana Alhamisi hii, Septemba 22 dhidi ya
Umoja wa Mataifa mjini Bujumbura, mji mkuu wa Burundi, wakilaani ripoti
ya Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya haki za binadamu nchini humo.
Waandamanaji,
miongoni mwao walikuwa Watutsi na Wahutu, makabila makuu nchini
Burundi, wameelezea kwamba ripoti ya hivi karibuni ya Umoja wa Mataifa
imejaa uongo na uzushi. Ripoti ya Umoja wa Mataifa imeonya kuwa huenda
kukatokea nchini Burundi mauaji ya kimbari, iwapo jumuiya ya kimataifa
haitokua makini, kwa hali inayoendelea kushuhudiwa nchini Burundi.
"Hakuna
kudanganywa", "Hakuna mauaji ya kimbari nchini Burundi", hayo ni baadhi
ya maneno waliyokua wakiyatamka waandamanaji hao.
"Tumekuja
kuonyesha hasira zetu dhidi ya ripoti ya Umoja wa
Mataifainayothibitisha kwamba mauaji ya kimbari yamo mbioni kutokea hapa
nchini Burundi. uchunguzi huu si wa kweli", ameshutumu mmoja wa
waandamanaji.
Ripoti hiyo iliyotolewa wiki hii inamtuhumu vikosi vya usalama vya Burundi kuwa vilihusika katika "mauaji kwa kiasi kikubwa."
Wachunguzi
huru wa Umoja wa Mataifa walioendesha uchunguzi huo wanabaini kwamba
tishio la mauaji ya kimbari liko katika kiwango cha juu nchini Burundi.
Serikali ya Burundi imeelezea kuwa ripoti hiyo imeandikwa kwa "shinikizo la kisiasa".
"Ripoti
hiyo inasema ukweli. Inaonyesha ukweli ambao raia wa Burundi wanapitia,"
amesema mmoja wa waangalizi wa siasa ya Burundi.
"Kwa ujumla, waandishi wa ripoti hiyo wana taarifa zote. Wamekua wakiuliza watu wengi,"ameongeza.
Hayo
yakijiri Wizara ya Mambo ya Ndani imewataka Wakuu wa mikoa na viongozi
wa tarafa, kwa ushirikiano na vikosi vya usalama, kila mmoja katika eneo
analoongoza, kuandaa maandamano Jumamosi wiki hii dhidi ya Umoja wa
Mataifa kwa kulaani ripoti ya umoja huo kuhusu hali ya haki za binadamu
nchini humo.
Machafuko
yaliyosababisha vifo vya watu wengi yalitokea nchini Burundi kufuatia
uamuzi wa Rais Pierre Nkurunziza, mwezi Aprili mwaka 2015, wa kuwania
muhula mwingine wa urais.
RFI
No comments:
Post a Comment