Mkuu wa wilaya ya Handeni Mh. Godwin Gondwe akisalimiana na mkazi wa kijiji cha nyasa.
Mkuu waa
Wilaya ya Handeni,Mh Godwin Gondwe Juzi alifanikiwa kusuluhisha mgogoro
wa mpaka uliokuwa ukivihusisha vijiji viwili vya kata ya kang’ata
wilayani Handeni .Vijiji hivyo ni Madebe na Nyasa ambao walikua
hawafahamu mpaka wao unaishia wapi,suluhu hiyo ilifanikiwa kumalizwa na
mkuu wa wilaya na mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya
Handeni ,Bwa.William Makufwe.
DC Gondwe
pia aliwataka wananchi na viongozi wajikite katika shughuli za
kimaendeleo badala ya kujikita kwenye suala la mipaka ,Kwa madai wapate
maeneo ya kulima wakati wakigombania maeneo ili wauze. Amewaonya
wasiuze ardhi kiholela na kufanya vizazi vijavyo kuwa watumwa kwenye
ardhi yao.

Mkuu wa
wilaya Mh.Godwin Gondwe akimsikiliza Mkurugenzi mtendaji wa wilaya ya
Handeni,Ndugu William Makufwe (pichani kushoto) akitoa ufafanuzi kwa
wananchi wa vijiji vya nyasa na madebe.

Mwenyekiti
wa kijiji cha nyasa na madebe wakipeana pongezi baada ya kujua mipaka
yao huku wakisistizwa kujikita zaidi katika masuala ya maendeleo.

Mkuu wa
wilaya ya Handeni Mh. Gondwe akipeana mkono wa pongezi na Mwenyekiti wa
kijiji cha Nyasa baada ya kupata mpaka wa maeneo yao.

Mkuu wa wilaya ya handeni Mh.Gondwe akizungumza na wananchi wa vijiji vya nyasa na madebe akiwakataza wasiuze ardhi kiholela na wasigombanie maeneo ili wayauze.
No comments:
Post a Comment