Hillary Clinton amesema kuwa anasikitika kuwa aliwataja mashabiki wa
mgombezi wa Republican, Donald Trump, kama kundi la watu wasiostahili
heshima.Katika taarifa kwa waandishi wa habari mgombezi huyo wa Urais kwa chama
cha Republican alisema kuwa kuna Wamarekani wengi wanaochapa kazi kwa
bidii wanaoamini kuwa wamepuuzwa na wanasiasa nchini.
Hata hivyo alisema kuwa ataendelea kukebehi watu wenye madharau ubaguzi wa rangi.
Meneja Mkuu wa kampeni wa Bwana Trump alikuwa amemlaumu Bi Clinton kwa
kile alichokitaja kama matusi dhidi ya mamilioni ya raia wa Marekani
aliposema kuwa wale wanaomwunga mpinzani wake walikuwa wabaguzi wa
rangi, wapinzani wa kijinsia, maaduni wa wapenzi wa jinsia moja na
wanaochukia Waislamu.
No comments:
Post a Comment