Zoezi la upimaji uzito likifanyika kupitia mpango wa AfyaKwanza.
Mkurugenzi
Raslimali Watu wa TBL Group,Bw.David Magesse amesema mazingira ya
amani na utulivu kwa wafanyakazi katika taasisi yoyote ile yanachangia
ufanisi wa kazi na hamasa ya kujituma kwa wafanyakazi wake na alishauri
kuwa kuna umuhimu wa taasisi mbalimbali kutambua mchango wa familia za
wafanyakazi wake.
Bwana
Magesse aliyasema hayo wakati akizungumzia tukio la tamasha la familia
za wafanyakazi wa kampuni ya hiyo lililofanyika jijini Dar es Salaam
ambalo liliwakutanisha wafanyakazi wa kampuni hiyo kanda ya Dar es
Salaam pamoja na familia zao ambapo walishinda na familia zao siku
nzima na kufurahi kwa pamoja.
“Sisi
kama kampuni yenye viwanda siku hii ni muhimu kwetu kwa kuwa
inatukutanisha katika mazingira ya nje ya ofisi na inatupa nafasi ya
kufahamiana zaidi sisi wenyewe na familia zetu na kujenga umoja zaidi na
utaratibu huu ni wa muhimu kwa waajiri wote kwa kuwa familia za
wafanyakazi zikiwa na amani na utulivu unawawezesha waajiriwa kufanya
kazi kwa ufanisi mkubwa”.Alisema.
Alisema
TBL Group inakahikisha katika kuongeza mori kwa wafanyakazi wake
inaandaa programu mbalimbali zinazoendana sambamba na kuhusisha familia
za wafanyakazi wake “Tunao mpango wa Afya Kwanza ambao tumekuwa
tukiutekeleza kwa kuhusisha pia familia za wafanyakazi ili kuwawezesha
kuwa na afya bora”.Alisema.
Bw.Magesse
alisema kuwa tamasha la familia la Dar es Salaam ni mwendelezo wa
matamasha ya familia ambayo tayari yamefanyika katika mikoa mbalimbali
ambako kampuni imewekeza katika mikoa ya Mwanza,Mbeya,Arusha na
Kilimanjaro na kuongeza kuwa kampuni inazidi kubuni programu za
kuwaweka karibu wafanyakazi wake pia kuziweka karibu familia zao.
No comments:
Post a Comment