RC Iringa Amina Masenza
Na MatukiodaimaBlog
Ndugu Wananchi wa Mkoa Iringa,
Ndugu Wananchi wa Mkoa Iringa,
Ndugu Waandishi wa Habari,
Mabibi na Mabwana.
Nachukua
fursa hii kueleza umma kwa muhtasari utekelezaji wa ilani ya ccm ya
mwaka 2015 kwa kipindi cha januari hadi juni, 2016 katika Mkoa wa
Iringa.Taarifa hii ni sehemu ya utekelezaji ambayo ilianza mwaka 2015.
Ndugu
Wananchi, shughuli zilizo tekelezwa kwa kipindi hicho zimefanikishwa kwa
kuunganisha nguvu za Serikali kuu,Serikali za Mitaa,Wahisani
mbalimbali,Sekta binafsi, Wananchi wenyewe na Mashirika yasiyo ya
Kiserikali.Tunawashukuru wadau wote kwa michango yao.
Ndugu Wananchi, Taarifa hii imetoa maelezo ya utekelezaji na mafanikio yaliyopatikana kwa kipindi husika kama ifuatavyo;
1. Kuongeza mapato ya ndani IBARA (20)
Mapato ya
ndani yaliyokusanywa ni shilingi 12,767,482,352 ambayo ni sawa na
75.7 ya lengo la shilingi 16,830,702,000 kwa mchanganuo ufuatao;
Kilolo DC 2,180,060,181, Iringa MC 3,526,582,802.93, Mufindi DC 2,837,351,416, Mafinga TC 1,580,742,133, Iringa DC 2,642,745,819
(e) ii Uhamasishaji umefanyika na jumla ya kaya 52,507 zimejiunga na mfuko wa afya ya jamii kwa mchanganuo ufuatao;
Iringa MC 9,385, Iringa DC 19,929,Mufindi DC 9,491, Mafinga TC 2,090, Kilolo DC 11,612
2. Kilimo na Ushirika IBARA (22)
(a) Kuongeza upatikanaji wa pembejeo na kusimamia matumizi ya pembejeo za ruzuku kwa kaya
Halmashauri
zote zilipokea pembejeo na kusimamia ugawaji wa pembejeo kwa kutumia
mfumo wa vocha ambapo jumla ya vocha 228,000 zimetolewa kwa kaya 76,000
kwa mchanganuo ufuatao; Iringa MC vocha 13,680 kwa kaya 4,560,
Iringa DC vocha 75,240, kwa kaya 25,080, Kilolo DC vocha 57,000 kwa
kaya 19,000,Mafinga TC vocha 22,800 kaya 7,600 na Mufindi DC vocha
59,280 kwa kaya 19,760
(d)ii Kuwezesha vikundi 15 vya Wakulima kuzalisha mbegu za kuazimia ubora (QDS).
Jumla ya
vikundi 9 vya Wakulima wa kuzalisha mbegu za kuazimia ubora (QDS)
vimewezeshwa kwa mchanganuo ufuatao; Kilolo DC 4 na Mafinga TC vikundi 4
na Mufindi DC 1
(d)iv Kuimarisha vikundi vya vijana kwa kuvipatia mafunzo.
Jumla ya
wakulima 359 wamepatiwa mafunzo ya viuagugu katika Kilimo ambapo kati
yao vijana 224 na wanawake 135 kwa mchanganuo ufuatao;
Manispaa -wanawake 97 na vijana 49, Kilolo DC- vijana 127 na wanawake 18 Mafinga TC- Vijana 48 na Wanawake 20.
(g)i Kujenga masoko 2 na maghala 5.
Maghala 2
ya kuhifadhia mazao katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa yanaendelea
kujengwa ambapo hali ya ujenzi imefikia asilimia 45
3. Mifugo (IBARA25)
(e) Kuanzisha mashamba darasa 18 ya malisho.
Jumla ya
mashamba darasa 15 ya malisho yameanzishwa ili wafugaji wa asili
wajifunze jinsi ya kuboresha na kuhifadhi malisho (feed banks) hususan
wakati wa kiangazi na ukame kwa mchanganuo ufuatao; Iringa MC 1, Iringa
DC 7, Mufindi 4 na Kilolo 3
(g) Kutoa elimu kwa wafugaji.
Elimu imetolewa kwa wafugaji 253 kwa mchanganuo ufuatao Iringa DC 93 , Kilolo DC 54, Mufindi DC 71 na Mafinga TC 36 (P.T)
4. UVUVI (IBARA 27)
(K) kuiendeleza Sekta ya Uvuvi
Jumla ya
vikundi vitano (5) vya vijana (3) na wanawake (2) vya ufugaji wa samaki
vimeanzishwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Halmashauri
nyingine zinaendelea na uhamasishaji.
(L) Ujenzi mabwawa ya samaki
Jumla ya
mabwawa ya samaki 20 yamejengwa kwa kushirikiana na wadau wa ufugaji
samaki ili kuongeza uzalishaji wa samaki kwa mchanganuo ufuatao; Iringa
MC 1, Mafinga TC 2,Iringa DC 17
5. Utalii (IBARA 29)
(e) Kuongeza idadi ya wananchi wanaotembeela vivutio vya utalii.
Jumla ya
Wananchi 1300 wametembelea vivutio vya utalii kwa mchanganuo ufuatao;
Iringa MC 410, Iringa DC 210, Kilolo DC 320 na Mufindi DC 360
6. Sekta ya Maliasili(IBARA 29)
(d)ii Kuongeza idadi ya mizinga ya kisasa ya nyuki
Jumla ya
mizinga 17,715 ya kisasa ya nyuki imeongeka kwa mchanganuo ufuatao;
Iringa MC 205, Mufindi DC- 5717, Kilolo DC 7790 na Iringa DC 4,003.
(f) Kuongeza eneo la kupanda miti.
Jumla ya
hekta 11,792.65 za eneo la kupanda miti limeongezeka kwa mchanganuo
ufuatao; Iringa MC hekta 200, Kilolo DC hekta 11,213, Iringa DC hekta 12
na Mafinga TC hekta 367.6.
7. Sekta ya Ardhi (IBARA 37).
(a)iv Kuongeza upimaji wa viwanja.
Jumla ya viwanja 494 na mashamba 3,778 yamepimwa kwa mchanganuo ufuatao;
Iringa
MC viwanja 183, Mufindi DC Mashamba 2124, Kilolo DC Mashamba 475,
Mafinga TC viwanja 300 na Iringa DC viwanja 11 na mashamba 1,179.
(a)viii Kutoa elimu kwa Vijiji 360 na Mitaa 222 juu ya Sheria za Ardhi na Sheria ya Mipangomiji
Elimu
imetolewa kwa Vijiji 19 na Mitaa 9 juu ya Sheria za Ardhi na Sheria ya
Mipango miji kwa mchanganuo ufuatao; Iringa MC Mitaa 5 , Mufindi DC
Vijiji 8, Kilolo DC Vijiji 5 Mafinga TC-Mitaa 4 na Iringa DC Vijiji 6.
(a)ix Kuanzisha na kuyaendeleza mabaraza ya ardhi
Jumla ya
Mabaraza ya Ardhi 52 yameundwa ili kufanikisha suala la utatuzi wa
migogoro ya ardhi kwa mchanganuo ufuatao; Iringa MC 18, Mufindi 4,
Kilolo DC 23, Mafinga TC 5 na Iringa DC 2
8. Utayarishaji wa Mipango ya Matumizi Bora ya ardhi nchini (IBARA 37 B)
(b)iv Kuongeza kasi ya utoaji wa Hatimiliki za Kimila
Jumla ya
hati miliki za kimila 3,926 zimetolewa kwa Wananchi kwa mchanganuo
ufuatao; Mufindi DC 1,882, Kilolo DC 865 na Iringa DC 1,179
(b)v kuongeza kasi ya utoaji wa Hatimiliki
Jumla ya
hatimiliki 1460 zimetolewa kwa mchanganuo ufuatao;Iringa MC 1020,
Mufindi DC 14, Kilolo DC 67, Mafinga TC 304 na Iringa DC 55
9. Nyumba (IBARA 37 (C))
(b)ix Kuelimisha na kuhamasisha wananchi kujenga nyumba bora
Elimu
imetolewa kwa Vijiji 8 na Mitaa 36 juu ya ujenzi wa nyumba bora kwa
mchanganuo ufuatao; Iringa MC Mitaa 20, Mufindi DC Vijiji 3, Kilolo DC-
Vijiji 5 , Mafinga TC- mitaa 16
10. USAFIRISHAJI NA UCHUKUZI (IBARA 39)
(b)ii Kujenga barabara za lami na changarawe
Jumla ya
km 28.06 za kiwango cha lami na km 285.5 za kiwango cha changarawe
zimetengenezwa kwa mchanganuo ufuatao; Iringa MC ( lami km 4.09 na
changarawe 2.5), Mufindi DC (lami Km 14.973 na changarawe Km 98)
,Kilolo DC (lami km 1 na changarawe km.156) Mafinga TC changarawe km
23 , Iringa DC ( Lami km 8 na changarawe km 29)
11. AFYA (IBARA 49)
(a) (i)
Jumla ya Hospitali mbili (2), zahanati (21) na vituo vya afya (6)
vinaendelea kujengwa kwa mchanganuo ufuatao ; Iringa MC Hospitali (1),
Kilolo DC Hospitali (1), Vituo vya afya (5) na Zahanati (14). Mafinga TC
Zanahati (4 ), Iringa DC kituo cha afya kimoja (1) na Zahanati(3)
12. AFYA (IBARA 50)
(b)i
Jumla ya vyandarua 420,545 vimegawiwa kwa Wananchi kwa mchanganuo
ufuatao; Iringa MC 42,589, Mufindi DC 146,634, Mafinga TC 44,556 na
Iringa DC 186,766
(b)v Usambazaji wa dawa umefanyika katika vituo 159 kwa mchanganuo ufuatao;
Iringa MC 21, Mufindi DC 62, Iringa DC 76
(P) Jumla
ya wazee 17,625 wametambuliwa na kupewa matibabu bure kwa mchanganuo
ufuatao; ; Iringa MC 1386, Mufindi DC 14,558, Kilolo DC 200 na Iringa DC
1,481
(q)v
vituo 105 vimepelekewa Dawa za kupunguza makali ya VVU na vifaa tiba kwa
mchanganuo ufuatao; Iringa MC 16 , Mufindi DC 22 na Iringa DC 67
13. HUDUMA ZA JAMII (IBARA 52)
(a)i Elimu ya awali
Jumla ya
watoto 33,708 wa elimu ya awali wameandikishwa kati ya lengo la
kuandikisha watoto 28,712 kwa mchanganuo ufuatao; Iringa MC 3,283,
Mufindi DC 9,740, Kilolo DC 8,390, Mafinga TC 1,546 , Iringa DC 10,749
(a)i Kuongeza idadi ya madawati
Jumla ya
madawati 24,533 yametengenezwa kati ya lengo la kutengeneza madawati
29,347 Madawati hayo yametengenezwa kwa mchanganuo ufuatao; Shule za
Msingi Madawati 21,304 na Shule za Sekondari Madawati 3229,
(a)iii kuhakikisha wanafunzi wote waliofaulu mtihani wa darasa la VII wanaendelea na kidato cha kwanza kwa 100%.
Wastani
wa 94.5% wa wanafunzi waliofaulu mtihani wa darasa la VII wamendelea
na kidato cha kwanza kama ifuatavyo; Iringa MC 99.02%, Mufindi DC 98%,
Kilolo DC 92%, Iringa DC 89.2% .
(d)vi Kuendela kujenga matundu ya vyoo kwa ajili ya wanafunzi wa shule za Sekondari.
Jumla ya matundu ya vyoo 96 yamejengwa katika shule za sekondari kwa mchanganuo ufuatao; Iringa MC 8, Kilolo DC 40, Iringa DC 48.
(d)viii Kuendelea kusimamia na kuimarisha michezo shuleni
Mashindano ya yanayohusisha shule za Sekondari (UMISSETA) yamefanyia katika ngazi ya Wilaya na Mkoa.
14. Maji (IBARA 54)
(a)Kuboresha huduma ya Maji Vijijini
Upatikanaji
wa huduma ya maji safi na salama umefika asilimia 71.2 na utekelezaji
wa miradi yote ya maji ni kama ifuatavyo;Iringa MC upo phase ya kwanza,
Mufindi DC umefikia 30%. Iringa DC Mradi wa Maji Kikombwe na Weru
umefikia 95%, Mradi wa Maji Mfyome umefikia 80%, Mradi wa Maji
Malinzinga umefikia 60%
(b)i Kuboresha huduma ya Maji Mijini.
Uboreshaji na upanuzi wa mitandao ya maji eneo la makao makuu ya Mkoa umefikia asilimia 97.
(b)Viii Kuongeza kasi ya ujenzi wa miundombinu ya utoaji wa majitaka
Halmashauri
ya Manispaa inaendelea na kazi ya ujenzi na ugawaji wa wateja kwenye
mfumo wa majitaka kazi hii inafanywa na taasisi ya IRUWASA ambapo
imefikia 16.5%.
15. UWEZESHAJI WA WANANCHI KIUCHUMI (IBARA 57)
(b)Jumla
ya vikundi vya ujasiliamali na VICOBA 873 katika Mitaa 26 na vijiji
41 vimetambuliwa na kusajiliwa kwa mchanganuo ufuatao; Iringa MC 741
katika Mitaa 20, Mufindi DC 83 katika Vijiji 17, Mafinga TC- vikundi
132 katika Mitaa 6, Iringa DC vikundi 49 katika vijiji 24.
(b)ii Kutoa mikopo kwa vikundi vya wanawake na vijana
Jumla ya
vikundi 152 vya wanawake na vijana vimepatiwa mikopo kwa mchanganuo
ufuatao;Iringa MC Wanawake 6 vijana 4, Mufindi DC wanawake 28 vijana
28, Mafinga TC wanawake 5, Iringa DC wanawake 41 vijana 40.
(b)iii Kutoa mafunzo ya ujasiliamali kwa vikundi vya wanawake 170, vikundi 45 vijana
Jumla
mafunzo ya ujasiliamali yametolewa kwa vikundi 243 kama ifuatavyo;
Iringa MC-Jumla ya vikundi 17, Mufindi DC wanawake 73 na vijana 17,
Mafinga TC wanawake 15 na vijana 6, Iringa DC wanawake 81 na vijana 34
16. KUENDELEZA MAKUNDI MAALUMU (IBARA 165)
Kuwatambua wazee na kuwapa huduma ya matibabu katika vijiji ,mitaa na vitongoji.
Jumla ya
wazee 17,625 wametambuliwa na kupewa matibabu bure kwa mchanganuo
ufuatao; Iringa MC 1386, Mufindi DC 14,558, Kilolo DC 200 na Iringa DC
1,481
17. WALEMAVU (IBARA 166)
Kuendelea Kuwatambua na kuwalinda walemavu wote wakiwemo wenye elemavu wa ngozi katika vijiji,mitaa na Vitongoji.
Jumla ya walemavu 151 wametambuliwa na kulindwa kwa mchanganuo ufuatao; Iringa MC 22, Mufindi DC 81 na Mafinga TC 48.
18. WANAWAKE (IBARA 167)
Kuhamasisha wanawake kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika ngazi zote katika vijiji
Elimu kwa
wanawake ya kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika ngazi zote
imetolewa katika Mitaa 49 na vijiji 41 kwa mchanganuo ufuatao; Iringa
MC Mitaa 38, Mufindi DC vijiji 20, Kilolo DC vijiji 10, MafingaTC Mitaa 6
na Iringa DC vijiji 11
19. WATOTO (IBARA 169)
Kuendelea kutoa elimu juu ya sheria ya mtoto ya mwaka ya 2009
Elimu juu ya sheria ya mtoto ya mwaka 2009 imetolewa kama ifuatavyo; Mafinga TC Mitaa 5, Mufindi DC kata 19.
20. VIJANA (IBARA 171)
Kufanya uraghibishi wa vijana ili waweze kujiari katika nyanja mbalimbali kama kilimo, ufugaji, ufundi sanaa
Uraghibishi
wa Vijana katika nyanja mbalimbali kama kilimo, ufugaji, ufundi sanaa
umefanyika katika Halmashauri zote kwa mchanganuo ufuatao;
Iringa MC Kata 10 Mufindi DC- Kata 3, Mafinga TC kata 7, Iringa DC kata 5 kilolo DC kata 1.
CHANGAMOTO KATIKA UTEKELEZAJI
Katika
utekelezaji wa ilani kwa kipindi husika Mkoa umeendelea kukabiliwa na
changamoto kadhaa ambazo kwa namna moja au nyingine zinafanya
utekelezaji wake kutofanyika kama ilivyokusudiwa.
· Uchakavu wa magari ambao unasababisha kuongezeka kwa gharama za kuyahudumia pamoja na uhaba wa vifaa vya kutendea kazi
· Ufinyu wa Bajeti kwa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa,Wakuu wa Wilaya na Halmashauri,
·
Ucheleweshaji wa kutolewa kwa fedha na kutotolewa kwa fedha pungufu kwa
ajili ya utekelezaji wa miradi ya Maendeleo zilizoidhinishwa kutoka
Hazina.
Mkoa, umejitahidi kuchukua hatua mbalimbali katika kukabiliana na changamoto hizo ikiwa ni pamoja na;
·
Kuongeza kiwango cha ukusanyaji wa mapato ya ndani katika Halmashauri
ili kupata fedha za kutosha kutekeleza miradi ya maendeleo kwenye
Halmashauri husika.
· Kuendelea kufuatilia hazina fedha ambazo hazijatolewa ili ziweze kutolewa
·
Kuendelea kuwashirikisha wadau mbalimbali chini ya mfumo wa PPP (Public
Private Partnership) katika kutekeleza shughuli mbalimbali.
TISHIO LA KUANDAMANA NA UVUNJIFU WA AMANI
Kanuni za Maadili ya Vyama vya Siasa zinatoa wajibu ambao unavifanya vyama vya siasa kuendesha shughuli zao kwa ustaarabu na uadilifu.
Ibara ya 5 ya Maadili hayo inaeleza kama ifuatavyo;
5.–(1)Kila chama cha siasa kitakuwa na wajibu
No comments:
Post a Comment