Monday, August 15, 2016

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI

KIDA
Jeshi la Polisi mkoa wa Mbeya limeendelea kufanya misako, operesheni na doria zenye tija katika maeneo mbalimbali ili kudhibiti uhalifu na wahalifu na limekuwa likishirikiana na wananchi na wadau wengine katika jitihada hizo za kukabiliana na uhalifu na wahalifu na kupata mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kupungua kwa matukio makubwa ya uhalifu na kumakata mali mbalimbali kama ifuatavyo :

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya mnamo tarehe 07.08.2016 hadi tarehe 13.08.2016 lilifanya misako mbalimbali katika maeneo ya Jiji la Mbeya. Misako hiyo ilifanyika maeneo ya Uyole, Isyesye, Ituha, Iyela, Airport, Kalobe, Nzovwe, Simike, Forest Mpya na Mwanjelwa. Katika Misako hiyo iliyolenga kukomesha vitendo vya wizi na uvunjaji nyumba wakati wa usiku  na mchana, mali na vitu mbalimbali vya wizi vilipatikana pamoja na watuhumiwa 10 kukamatwa kuhusika katika matukio hayo.


Mafanikio yaliyopatikana katika misako:

KUPATIKANA NA RISASI 10 ZA SMG
Mnamo tarehe 14.08.2016 majira ya saa 14:00 mchana huko maeneo ya Sae Jijini Mbeya, Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la JOHAN MWASUMBWI (32) Mfanyabiashara na Mkazi wa Sae alikamatwa akiwa na risasi 10 za silaha aina ya SMG kinyume cha sheria.

KUPATIKANA NA SARE ZA JESHI [JWTZ]

Mnamo tarehe 14.08.2016 majira ya saa 14:00 mchana huko maeneo ya Sae Jijini Mbeya, Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la JOHAN MWASUMBWI (32) Mfanyabiashara na Mkazi wa Sae alikamatwa akiwa amevaa sare za JWTZ aina ya Kombati [Shati na Suruali].

Mtuhumiwa atafikishwa mahakamani mara baada ya uchunguzi kukamilika.

Kupatikana kwa Gari moja na Bajaji: Katika misako hiyo Bajaji nne zilipatikana zenye namba za usajili MC 999 AKQ, MC 250 ARG, MC 274 AAK na moja iliyokuwa na namba 28 ubavuni  pamoja na gari moja yenye namba ya usajili T.501 CAB aina ya Toyota Noah rangi nyeupe.

Kupatikana kwa Mali za Wizi: Katika misako hiyo, mali na vitu mbalimbali vya wizi vilipatikana ambavyo ni:-

  1. Vyerehani vitatu moja aina ya Butterfly,
  2. Amplifier moja,
  3. Spika tatu kubwa,
  4. Laptop aina ya Samsung,
  5. Laptop aina ya HP G.56,
  6. Laptop aina ya HP 693,
  7. Redio aina ya Panasonic,
  8. Television Flat Screen aina ya Boss inchi 32,
  9. Monitor aina ya HP,
  10. Mashine ya Kudarizi ya Umeme,
  11. Viti vitatu vya Plastic,
  12. Keyboard aina ya ACER na Mouse,
  13. Deki aina ya Samsung,
  14. Subwoofer moja aina ya Piano,
  15. Computer isiyokuwa na jina,
Vitu vingine vilivyopatikana ni pamoja na Simu 10 za aina mbalimbali ikiwemo Tecno, Samsung na Itel, Chaja ya simu ya Smartphone, Earphone 08, Betri za simu 07, Makava ya simu, Flash Disk 03, Katoni za Soda 10, Kreti za bia tupu 06, Kreti za soda 08 na bidhaa mbalimbali za dukani ambazo ni mafuta ya kula, mafuta ya kujipaka mwilini, biskuti, juice, sabuni za unga.
Kukamatwa Watuhumiwa 10 wa Uhalifu: Aidha katika misako hiyo watuhumiwa 10 walikamatwa kuhusika katika matukio ya kupatikana na mali za wizi na kuvunja nyumba usiku na kuiba ambapo majalada ya uchunguzi yalifunguliwa. Watuhumiwa hao ni pamoja na
  1. STEPHANO NAZMA (24) Mkulima na Mkazi wa Ituha
  2. REGINA BENEDICT (16) Mkulima na Mkazi wa Kalobe
  3. SHABANI DAFA (21) Dereva na Mkazi wa Airport
  4. GODFREY NDUKWA (22) Mfanyabiashara na Mkazi wa Airport
  5. JAMES ENOCK (20) Mkulima na Mkazi wa Airport.
Watuhumiwa wengine waliokamatwa ni
  1. FIDELIS NGOVANO (32) Mkulima na Mkazi wa Wilaya ya Mbarali
  2. ISRAEL LIYAUMI (33) Mkulima na Mkazi wa Madibila Wilayani Mbarali 8. ZEBEDAYO KADUMA (35) Mkulima na Mkazi wa Uyole
  3. RIZIKI ALFEO (17) Mkulima na Mkazi wa Ubaruku Wilayani Mbarali na 10. JOSHUA DAUDI (26) Mkulima na Mkazi wa Ubaruku Wilayani Mbarali.
Aidha katika zoezi hilo la Misako lilienda sambamba na ukaguzi wa nyumba za kulala wageni zilizopo katika maeneo ya Uyole, Isyesye, Ituha, Iyela, Airport ya Zamani, Kalobe, Nzovwe, Simike, Forest Mpya na Mwanjelwa. Hali kadhalika wamiliki na wahudumu katika Nyumba hizo za kulala wageni walipewa elimu ikiwa ni pamoja na kuandika majina ya wageni wote katika kitabu cha wageni pamoja na kuweka namba za wahudumu, wamiliki na viongozi wa Jeshi la Polisi kwenye milango kwa ajili ya dharura zitakazojitokeza kwa hatua zaidi.

WITO

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Naibu Kamishna wa Polisi DHAHIRI A. KIDAVASHARI anatoa wito kwa jamii hasa vijana kuacha tabia ya kutaka kupata mali au utajiri kwa njia ya mkato na badala yake wafanye kazi halali ili wapate kipato halali. Pia anasisitiza kuwa maendeleo hayapatikani kwa kufanya kazi hama biashara haramu, watumie fursa zilizopo Mkoa wa Mbeya kujitafutia ajira.
Imesainiwa na
[DHAHIRI A. KIDAVASHARI – DCP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA

No comments:

Post a Comment