Kiongozi
wa waasi, Riek Machar (kulia) na rais wa Sudani Kusini, Salva Kiir
(kushoto) Mei 9 mwaka 2014. Lakini, rais wa Sudani Kusini na mpinzani
wake, hawakusiriki katika mazungumzo ya amani, Addis Ababa, Ethiopia.
Rais wa
Sudan Kusini amesema Jumatatu hii kwamba atatahmini mpango wa Umoja wa
Mataifa wa kutuma askari 4,000 wa kulinda amani katika nchi yake ambayo
inakabiliwa na hali ya vurugu kati ya vikosi vya serikali na askari
wanaomuunga mkono Reik Machar.
Baraza la
Usalama la Umoja wa Mataifa siku ya Ijumaa lilipitisha azimio la
kuidhinisha kutumwa kwa kikosi cha ulinzi chenye askari 4,000 katika mji
wa Juba kama sehemu ya ujumbe wa kulinda amani nchni humo.
Kikosi
hiki, ambacho kinaundwa na askari wa Afrika, kitakua na kazi ya
kuhakikisha amani inarejea katika mji mkuu wa Sudan Kusini na kulinda
baadhi ya majengo muhimu kama uwanja wa ndege.
Msimamo
wa kwanza wa serikali ya Rais Salva Kiir ulikua kufutilia mbali mpango
huo kabla ya kurejelea upya msimamo huo mwishoni mwa wiki.
"Baadhi
ya watu wanaishtumu serikali ya mpito kukataa na kupambana na Umoja wa
Mataifa, jambo ambalo si kweli," amesema Salva Kiir katika sherehe
inayoshiria kuanza kwa kikao cha Bunge.
"Serikali
ya mpito bado haijakutana ili kueleza uamuzi wake wa mwisho.
Majadiliano yatafanyika ili kuamua msimamo wa mwisho," Rais Salva Kiir
ameongeza.
Umoja wa Mataifa umetishia Sudan Kusini kuichukulia vikwazo vya silaha kama serikali itakataa kutoa ushirikiano wake.
Shirika
la kimataifa la haki za kibinadamu la Human Rights Watch (HRW) limesema
kuwa limepata ushahidi wa mauaji ya kikatili ya raia, ikiwa ni pamoja na
mauaji ya mwandishi wa habari , aliyeuawa akiwa mikononimwa vikosi vya
usalama wakati wa mapigano yalitokea mwezi uliopita. HRW pia imebaini
visa vya ubakaji vilivyotekelezwa katika machafuko ya hivi karibuni.
RFI
No comments:
Post a Comment