TAMASHA
la wasanii wa kizazi kipya la kuchangia madawati limefanyika mwishoni
mwa wiki katika ukumbi wa Dar Live Mbagala ambapo jumla ya madawati 150
yamepatika.
Tamasha
hilo liliandaliwa na Mkuu wa Wilaya ya Handeni Godwin Gondwe ‘Double G’
ambapo aliwashukuru wasanii hao kwa kujitokeza kusapoti upatikanaji wa
madawati kwa watoto wa Handeni ambao ni moja ya changamoto zinazokabili
Wilaya yake ukiachilia ile ya Maji.
Wasanii
waliojitokeza kuunga mkono juhudi za Mkuu huyo wa Wilaya ya Handeni
walisema wameamua kumsapoti Gondwe kwa kuwa wanamfahamu muda mrefu toka
akiwa mtangazaji wa radio na alikuwa akiwasapoti kazi zao kwa kiasi
kikubwa.
Ben Paul
alisema “Wasanii kama wasanii tunatakiwa tusaidie jamii yetu kama hivi,
naishi kwenye jamii hivyo naona matatizo mengi yanayokabili jamii yetu
ni wajibu wangu kutumia nafasi hii kusaiii, karne hii wadogo zetu bado
wanakaa chini, tunatakiwa kushirikiana kwa pamoja kumaliza tatizo
hilo.”alisema Ben Paul anayetamba na Wimbo wake wa sasa wa ‘Moyo
Mashine’ na kuongeza.
“Vijana
wa sasa wanapenda kushinda kwenye mitandao ya kijamii na kulalamikia
serikali, wanataka serikali ndio iwafanyie kila kitu wakati sisi
hatufanyii jambo serikali.”alisema.
Msanii
nguli, Ambwene Yesaya ‘Ay’ akizungumzia tamasha hilo alisema “Double G
kwanza kabisa ni mtu wa watu, ndio maana wasanii wote unaotuona hapa
tumeamua kumsapoti bure kabisa, alivyotueleza wazo lake tukamwambia ni
zuri na tutamsapoti, alichokifanya ni kitu kizuri ambacho kinatakiwa
kiigwe na kila mtu.
“Itakuwa
vizuri kila mtu akaweka nia ya kusaidia sio lazima tutengeneze madawati
tunaweza tukafanya siku ya kuotesha miti ambayo naamini kila msanii
akiotesha mti mmoja leo, utakuwa na manufaa kwa vizazi vijavyo.”alisema
Ay.
Aidha
mwandaaji wa tamasha hilo Godwin Gondwe alisema kuwa Wilaya yake
inakabiliwa na uhaba wa madawati 530 na anashukuru kwa kupata madawati
150 katika fedha zilizopatikana kwenye tamasha hilo la Wasanii hna
kwamba bado ana upungufu wa madawati 380.
“Nawashukru
sana wasanii waliojitoa kunisapoti, na wakazi wa Wilaya ya Temeke
kujitokeza kumuunga mkono Rais wetu ili kutengeneza historia za wadogo
zao wasikae chini tena, na katika tamasha hili tumeweza kukusanya fedha
ambazo zitatuwezesha kupata madawati 150.”alisema Gondwe.
Katika
tamasha hilo, muitikio wa watu ulikuwa mkubwa na lilipendezeshwa na
wasanii mbalimbali. Walioanza kufanya makamuzi mwanzoni mwa tamasha hilo
ni pamoja na Bendi ya La Musica Vijana Classic, Mc wa Dar Live Brighton
‘Dalada’ na wengine wengi.
Baada ya
shoo kunoga mashabiki wa Dar Live walifurahia muziki mzuri kutoka kwa
Bendi ya Injili ya GWT (Glorious Worship Team), Mfalme wa Muziki wa
Uswazi maarufu kama Singeli Msaga Sumu, Sterio, Ben Pol, Linex huku Fid
Q, AY, Msami na Barnaba wakikamilisha listi kwa makamuzi ya nguvu.
No comments:
Post a Comment