Naibu waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali
za mitaa TAMISEMI Jafo Suleiman Said akisikiliza
kwa makini maelezo ya kilimo cha
mbogamboga yanayofanywa na Jeshi la kujenga Taifa JKT
Naibu waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali
za mitaa TAMISEMI Jafo Suleiman Said akiwa
kwenye picha ya pamoja na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama mara
baada ya kutembelea banda la Halmashauri hiyo
Naibu waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali
za mitaa TAMISEMI Jafo Suleiman Said akisikiliza
kwa makini maelezo ya awali kutoka kwa Mwenyeji wake katika Maonesho hayo
ambaye ni mkuu wa Wilaya ya ikungi
Miraji Jumanne Mtaturu
Naibu waziri TAMISEMI Jafo Suleiman Said akisaini kitabu cha wageni katika banda la Mwanzo Bora Nutrition Program
Mgeni na Mwenyeji wakifurahi kufuatia maandalizi mazuri
ya Maonesho ya Nane nane kanda ya kati Dodoma
Naibu waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali
za mitaa TAMISEMI Jafo Suleiman Said akisikiliza
maelezo ya namna ya kulima kilimo cha kisasa katika Banda la Halmashauri ya Wilaya ya kongwaNaibu waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI Jafo Suleiman Said akizungumza na Luteni AJ Massawe Meneja wa banda la JKT Naibu waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI Jafo Suleiman Said akipokea zawadi ya mafuta ya alizeti kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Deogratius Ndejembi
Naibu waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI Jafo Suleiman Said akiwa katika pichaya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya ikungi na Kongwa pamoja na watendaji Mfuko wa LAPF
Na Mathias Canal, Dodoma
Watanzania wametakiwa kuthamini na kununua bidhaa zinazozalishwa nchini Tanzania hususani katika sekta ya Kilimo, Ufugaji na uvuvi kwani hakuna sababu ya kuagiza bidhaa kutoka nje ya nchi ilihali bidhaa hizo wanazoagiza zinazalishwa na watanzania wenzao.
Naibu waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI Jafo Suleiman Said ameyasema hayo mara baada ya kutembelea baadhi ya mabanda katika maonyesho ya wakulima Nane nane Kanda ya kati Dodoma yanayofanyika katika uwanja wa Nzuguni huku kauli mbiu ya mwaka huu ikiwa ni "Kilimo, Mifugo na Uvuvi ni nguzo ya maendeleo, Kijana shiriki kikamilifu (Hapa Kazi Tu).
Jaffo amesema kuwa asilimia kubwa ya watanzania wamekuwa watumwa wa mambo ya kigeni, kuiga tamaduni mbalimbali ikiwemo matumizi ya bidhaa zinazotoka nje ya nchi wakati pia bidhaa hizo zinazalishwa nchini, huku akitolea mfano wa manunuzi ya viatu kutoka nchi mbalimbali wakati hapa nchini Jeshi la Magereza linatengeneza viatu bora vya ngozi tena kwa bei nafuu.
Sambamba na hayo pia Naibu Waziri huyo ameiagiza Mamlaka ya Ustawishaji Makao makuu Dodoma kusimamia vyema na kwenda na kasi kubwa katika utengenezaji wa stendi kubwa na ya kisasa ili kufanana na mji wa Dodoma ambapo pia hivi karibuni makao makuu ya serikali yatahamia mjini hapo.
Aidha ameongeza kuwa Maonesho hayo yanapaswa kuboreshwa ili maonyesho yajayo yawe ya kitaifa ambapo nchi mbalimbali zitapata fursa ya kutembelea na kuifanya Tanzania kujikomboa katika wimbi la umasikini.
Maonesho hayo yanahusisha Shughuli za wakulima, wafugaji wa mifugo, wafugaji wa nyuki, wavuvi, wana mazingira, wasindikaji wa bidhaa za mazao ya kilimo na mifugo, wizara taasisi/Makampuni ya umma, makampuni Binafsi, mabenki, taasisi za umma na za binafsi na mashirika yasiyo ya kiserikali.
Akitoa salamu za shukrani kwa niaba ya waandaaji wa Maonesho hayo Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida Miraji Jumanne Mtaturu amesema kuwa maandalizi ya maonyesho hayo yametumia muda mfupi lakini kwa kiasi kikubwa yamekuwa bora na kuahidi kuwa na Maonesho yajayo kuwa bora zaidi katika kipindi kinachokuja.
Mtaturu amesema kuwa lengo mahususi la maonesho hayo ni utoaji wa elimu ya matumizi ya teknolojia mbalimbali kwa wadau wengi kwa muda mfupi ambapo watajifunza kwa njia ya kuona, kujadiliana na kuulizana maswali.
Ameongeza kuwa maeneo makuu ya mafunzo ni teknolojia za uzalishaji wenye tija wa mazao, mifugo na usindikaji wa bidhaa ili kuongeza thamani.
Dc Mtaturu amesema kuwa pia wadau watajionea na kujifunza huduma zitolewazo na serikali, Mashirika ya umma na binafsi, ambapo wafanya biashara wanayatumia maonesho hayo kwa kuuza bidhaa, kufahamiana na kuingia makubaliano.
Kwa upande wake Katibu wa maandalizi ya Maonesho hayo Aziza Rajabu Mumba amesema kuwa Wanatarajia kila mwananchi atakayetembelea maonesho hayo kwenda kutekeleza kwa vitendo anayojifunza katika eneo lake na kuwafundisha wengine ambao hawakupata fursa ya kuhudhuria kwenye Maonesho hayo.
Aidha amesema Malengo ya muda mrefu ni kuendeleza uwanja wa Nzuguni ufikie ubora na hadhi ya viwanja vya maonesho ya Kilimo Kimataifa na kuendelea kushawishi wadau mbalimbali kuwekeza ili kuufanya uwanja wa Nzuguni uwe kituo cha huduma cha Maonesho ya Kilimo nchini kama ilivyo kwa uwanja wa Mwalimu Nyerere Dar es salaam kwa maonesho ya Biashara.
No comments:
Post a Comment