Mwenyekiti
wa Mtaa wa Sangabuye, kata ya Igombe wilayani Ilemela mkoani Mwanza
anayejulikana kwa jina la John Mayala anashikiliwa na polisi kwa kosa la
kumtorosha na kumpa ujauzito mwanafunzi.
Mwanafunzi
huyo amefahamika kwa jina la Lucy Daudi, anayesoma kidato cha pili
katika Shule ya Sekondari Sangabuye ambaye anakadiriwa kuwa na umri wa
kati ya miaka 14 hadi 17.
Aidha
jeshi la polisi pia linamshikilia mama mzazi wa mwanafunzi huyo aitwaye
Agnes Kadilana mwenye umri wa miaka 48 mkulima, mkazi wa Sangabuye kwa
kosa la kushindwa kutoa ushirikiano kwa polisi pindi alipohojiwa
kuhusiana na tukio hilo.
Inadaiwa kuwa mama huyo alishiriki katika kumtorosha binti yake kwenda kuishi kinyumba na mtuhumiwa baada ya kupewa fedha.
Mama
huyo amedai kuwa binti yake aliamua mwenyewe kuacha shule kwa madai
kuwa shule imemshinda. "Yeye mwenyewe alisema hawezi kusoma, akasema
ajifunze cherehani, sasa sijui" Amesema mama huyo.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mwanza DCP Ahmed Msangi ametoa wito kwa wakazi wa
mkoa huo hususani wanaume wenye tabia ya kuwa na mahusiano ya kimapenzi
na wanafunzi pamoja na wasichana wenye umri chini ya miaka 18 kuacha
mara moja kwani ni kinyume cha sheria bila kujali kama palikuwa na
makubaliano au la.
No comments:
Post a Comment