Halmashauri
ya wilaya ya Mufundi Mkoani Iringa imefanikiwa kutekeleza agizo la
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania katika ukusanyaji wa
mapato ya ndani, baada ya kukusanya zaidi ya Shilingi Bilioni 4.7 sawa
na asilimia 82.7 kati ya bilioni 5.6 ilizopanga kukusanya katika mwaka
wa Fedha 2015-2016.
Taarifa
ya kitengo cha habari na mawasilino cha halmashauri ya Wilaya ya
Mufindi, imetanabaisha kuwa, mafanikio hayo yamebainishwa na Mwenyekiti
wa halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Mh. FESTO MGINA kwenye kikao cha
kawaida cha baraza la madiwani wa halmashauri hiyo kilichoketi mjini
Mafinga.
MGINA
amesema, mafanikio hayo ni matokeo ya ufuatiliaji na usimamizi mzuri wa
vyanzo vya mapato vya halmashauri kama vile mapato yatokanayo na
usafirishaji wa mbao na Magogo, kuuzwa kwa sehemu ya msitu wa
halmashauri sanjari na ushuru unaokusanywa kwa wafanyabiashara wadogo
katika halmashauri hiyo.
Aidha,
Mwenyekiti huyo ameongeza kuwa, pamoja na kutekeleza agizo la Waziri
Mkuu la kila halmashauri kukusanya mapato kwa asilimia 80 na kuendelea,
kikwazo kikubwa cha kutofikia asilimia 100 ni kuzaliwa kwa halmashauri
ya mji wa Mafinga jambo amabalo lilisababisha kugawana vyanzo vya mapato
.
No comments:
Post a Comment