Na
Mathias Canal, Singida
Jeshi la polisi Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida
limemtia nguvuni Diwani wa Kata ya Iseke kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na
Maendeleo CHADEMA Emmanuely Njingu
kwa kosa la kukwamisha shughuli za serikali kwa kuzuia watendaji wa serikali
kufanya kazi yao ikiwemo ukusanyaji wa mapato.
Njingu ambaye alikuwa mjumbe wa kamati ya fedha
awali kabla ya kuwekwa nguvuni na jeshi la polisi alivuliwa ujumbe wa kamati
hiyo kutokana na kukiuka taratibu na makubaliano ya baraza la madiwani jambo
ambalo limepelekea kuhamishiwa katikakamati nyingine.
Akitoa taarifa ya kukamatwa kwa diwani huyo
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi ambaye ni Diwani wa Kata ya
Irisia Ally Juma Mwanga amesema kuwa
Diwani huyo amekamatwa kwa mujibu wa sheria hivyo yeye kama mwenyekiti hawezi
kuingilia taratibu, sheria,na kanuni za serikali.
Mwanga
amesema kuwa tarehe 19 mwezi Julai moja ya maadhimio ya kamati ya fedha na
vikao vya baraza ilikuwa ni kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri
lakini diwani huyo amekiuka makubaliano hayo kwa kung’oa mageti ya vizuizi vya
barabarani kwa ajili ya ukaguzi wa mazao jambo ambalo limepelekea kuzorota kwa ukusanyaji
wa mapato ya Halmashauri.
Ameongeza kuwa Mjumbe yeyote anayekiuka maazimio
wanayokubaliana na kutoa siri za kamati adhabu yake kisheriani kupoteza sifa ya
kuwa mjumbe wa kamati husika.
Amesema diwani huyo ameondoshwa katika nafasi hiyo baada
ya maridhiano ya kamati hiyo na kukubaliana kumuhamishia katika kamati nyingine
ya huduma za uchumi.
“Jambo mkishakubaliana kisheria tena kwenye vikao
vya kisheria maana yake linakuwa ni sheria hivyo kwa kiongozi yeyote akikiuka
taratibu za kisheria zinachukua mkondo wake, kanuni za Halmashauri ni za watu
wote hazichagui upande mmoja” Alisema
Mwanga
Hapo jana Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu alihutubia
Baraza la madiwani wa Halmashauri ya Wilaya hiyo ikiwa ni mara yake ya mwanzo
kabisa tangu alipochaguliwa na Rais John
Magufuli kuwa Mkuu wa Wilaya hiyo ambapo pamoja na kuzungumzia kuwepo kwa
changemoto ya uhaba wa maabara, afya duni na miundombinu pia alizungumzia
kuhusu ukusanyaji hafifu wa mapato jambo ambalo linairudisha nyuma Halmashauri
ya Wilaya hiyo.
Bajeti ya Wilaya ya Ikungi kwa Mwaka 2013/2014
ilikuwa na Shilingi 509,701,044 namakusanyoyakeyakawa ni 338,325,000 ambapo
hata hivyo mwaka ulimalizika kwa kuwa na upungufuwa shilingi 171,376,044.
Mwaka 2014/2015 ilipangwa bajeti ya shilingi
631,455,000 lakini makusanyo yake yakawa ni shilingi 457,555,172 ambapo mwaka
ulimalizika kwa kukusanya 173,899,828.
Mwaka wa bajeti 2015/2016 bajeti ya Halmashauri
iliyopangwa ilikuwa ni shilingi 1,127,030,000 makusanyo yalikuwa ni 679,283,000
ambapo hata hivyo mwaka ulimalizika kwa kwa kuwa na upungufu wa shilingi 450,747,000
hivyo kwa miaka mitatu Halmashauri hiyo imeshindwa kufikia malengo ya
ukusanyaji.
Mwanga amesema kuwa Kutofikiwa malengo hayo
kumesababishwa na kutopewa ushirikiano watendaji katika ukusanyaji wa mapato
hii ikiwa ni kufuatia kauli za mazuio zinazotolewa na baadhi ya wanasiasa.
Hata hivyo ametoa Mwito kwa viongozi wa serikali,
wanasiasa, taasisi za dini na wananchi kushirikiana kwa pamoja ili kufikia
malengo ya kuifanya Ikungi kukua kiuchumi .
No comments:
Post a Comment