Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo mkoa wa Morogoro, Agnes
Mkandya amemwaga machozi alipokuwa akiulizwa maswali na Kamati ya Bunge
ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC).
Tukio
hilo lilitokea jana wilayani humo baada ya kamati hiyo kumuuliza
Mkurugenzi huyo maswali mbalimbali ikiwa ni pamoja na udanganyifu na
ubadhirifu wa fedha mkubwa unaoonekana kufanywa na baadhi ya watumishi
wa Halmashauri hiyo.
Swali
lililomliza Mkurugenzi huyo liliulizwa na Mbunge wa viti maalum, Leah
Komanya (CCM), aliyetaka majibu kuhusu wizi wa mapato kwa njia
mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutumia karatasi maalum, unaofanywa na
watendaji hao.
Mkurugenzi
huyo alikiri kuwepo ubadhirifu mkubwa wa fedha ndani ya Halmashauri
hiyo na kueleza hatua alizochukua, huku akijitetea kuwa yeye ni mgeni
hivyo mambo mengi bado hajayafanyia kazi.
“Kamati
ielewe kwanza Halmashauri ya Gairo imeoza na ni chafu kwa sababu kuna
ubadhirifu mkubwa. Tayari nimewasimamisha kazi watumishi tisa wa idara,
lakini kumbukeni na mimi ni mgeni sina muda mrefu,” alijibu Mkurugenzi huyo kabla ya kuanza kumwaga chozi.
Wajumbe
wa Kamati hiyo wakiongozwa na mwenyekiti wake, Vedastus Ngombale Mwiru
walimtuliza kwa kumbembeleza wakimtaka aondoe woga kwani ni maswali ya
kawaida aliyoulizwa.
Baada
ya hali hiyo, Mwenyekiti huyo aliamuru majibu ya maswali hayo na
mengine kutolewa na Mkaguzi wa Ndani wa Halmashauri hiyo kwakuwa yeye
alikuwepo muda mrefu.
No comments:
Post a Comment