Mamlaka
ya Mapato Tanzania TRA imewataka wafanyabiashara katika jiji la Dar es
salaam kuboresha taarifa za usajili wa namba ya utambulisho wa mlipa
kodi (TIN) ili kuondokana na mfumo wa kizamani wa usajili wa namba hiyo.
Uhakiki
huo utaiwezesha mamlaka hiyo kuweza kujua idadi sahihi ya
wafanyabiashara walipa kodi, kuondoa walipa kodi hewa ambao wamekuwa
hawajihusishi na biashara kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo vifo au
kufungwa kwa makampuni yao.
Akiongea
na waandishi wa habari jana jijini Dar es salaam, Kamishna Mkuu wa
Mamlaka ya Mapato Tanzania ndugu Alphayo Kidata alisema mfumo huo
utawawezesha wafanyabiashara kulipa kodi kwa gharama nafuu sambamba na
kuweka mazingira ya ulipaji kodi kwa hiari.
Kidata
alisema kuwa mfumo wa sasa wa uhifadhi kumbukumbu za walipa kodi
ulikuwa na kasoro nyingi hivyo mfumo mpya utaendana na ukuaji wa
teknolojia na kukuza uchumi.
“Zoezi
hili linamtaka kila mwenye namba ya utambulisho yani TIN kufika katika
ofisi za TRA zilizopo karibu naye bila kuwakilishwa na mtu yeyote na
zoezi litatumia dakika 10 kumalizika” alisema
Naye
Elija Mwandubya ambaye ni kamisha wa mapato wa ndani wa mamlaka hiyo,
alisema zoezi hilo litachukua siku 60 na kuanzia Dar es salaam na
baadaye kuhamia mikoa mingine ndani ya nchi.
“TRA
ina wafanyabiashara walipa kodi milioni mbili na laki moja hivyo
uboreshwaji wa TIN utatupa uelewa wa idadi kamili ya walipa kodi” Alisema
Elija
alisema kutakuwa na vituo maalum kwaajili ya uhakiki wa taarifa katika
mikoa ya kikodi ambapo Kinondoni wafanyabiashara watatakiwa kutembelea
ofisi za TRA zilizopo jengo la LAPF – Kijitonyama na Kibo Complex
Tegeta.
Ilala wafanyabiashara watembelee ofisi ya TRA shauri moyo na 14 Rays Gerezani na Temeke wafike ofisi za uwanja wa Taifa.
No comments:
Post a Comment