Monday, August 15, 2016

MAMA SARA MMBAGA APOTEA, MSAADA KWA ATAKAYE MUONA ATOE TAARIFA POLISI

SAR
Mama Sara Mmbaga (pichani) anatafutwa na Mtoto wake kipenzi kwani amepotea tangu mwaka jana Oktoba 26, 2015 huku juhudi kubwa ya kumtafuta inayofanywa na Binti yake Sarafina aliyepo nchini Marekani, ndugu na jamaa zikiwa bado hazijafanikiwa.

Mara ya mwisho Mama Sara Mmbaga alionekana maeneo ya Mbezi Makonde, Mtaa wa Bunge Road, Jijini Dar e Salaam akiwa ameongozana na Mwanaume ajulikanaye kwa jina la Gamaeli Mwasumbi maarufu kwa jina la “Gama” mwenyeji wa Mbezi Beach.

Tangu siku hiyo ya Jumapili tarehe 26 Oktoba, 2015 alitoweka kusikojulikana huku vitu vyake vilivyokuwepo kwenye nyumba yake aliyokuwa anaishi vikiwa vimeondolewa.

Aidha, Juhudi mbalimbali za kumtafuta mama Sara Mmbaga zimefanyika bila mafanikio tangu alipopotea ambapo taarifa ya kupotea kwake ziliripotiwa katika Kituo cha Polisi Kawe pamoja na vituo mbalimbali vya Habari hapa nchini.

Tunaomba watu, mtu yeyote atayeweza kumuona basi anaweza kutoa taarifa kituo cha Polisi kilichokaribu naye. 

Tunajua ni jinsi gani maumivu anayoyapata Mtoto wake kipenzi wa pekee Sarafina lakini tunamuombea kwa Mungu amlinde huko aliko na Malaika wake wamrudishe Mama Sara akiwa salama salimin kwenye himaya yake.

Tunapenda kumwambia Sarafina kuwa aendelee kumwamini Mungu kwa maana kila hatua azikabidhizo kwake na kumwamini basi Mungu atamtendea muujiza.

No comments:

Post a Comment