Friday, August 5, 2016

Mahabusi waliojaribu kutoroka watiwa mbaroni


Mahabusi wawili kati ya saba waliotoroka chini ya ulinzi wa askari wa Jeshi la Polisi katika eneo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Kilimanjaro, wametiwa mbaroni na kuhukumiwa kutumikia vifungo jela.

Kutoroka kwa mahabusi hao kulisababisha askari 10 mkoani Kilimanjaro waliokuwa wakiwalinda kushikiliwa na polisi kwa mahojiano.

Mahabusi hao ni Lucas Akaro (26) ambaye alijisalimisha kwa uongozi wa Gereza la Karanga na Charles Malenge (24), aliyekamatwa na Polisi akiwa amejificha nyumbani kwake.

Wakati wakitoroka, Akaro alikuwa akikabiliwa na kesi ya mauaji ya mwanafunzi wa mwaka wa tatu chuo cha udaktari KCMC, Baneti Materu (22) na Malenge  ya unyang’anyi.

Mahabusi hao walifikishwa kortini jana mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Joachim Tiganga na kukiri shtaka moja kati ya mawili yaliyokuwa yakiwakabili.

No comments:

Post a Comment