NAIBU
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi
Kingwangalla ameagiza Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam kumkamata
tabibu maarufu Juma Mwaka ndani ya saa 24
Dk.
Kigwangalla ametoa amri hiyo leo jijini Dar es Salaam alipokitembelea
tena kituo cha Fore Plan kinachomilikiwa na tabibu huyo maarufu kwa jina
la ‘Dk. Mwaka.’
Serikali
ilitangaza kukifungia kituo hicho cha afya na vingine vitatu mwezi
mmoja uliopita kwasababu zilizoelezwa kuwa ni kutoa huduma kinyume na
sheria ambapo kituo cha tabibu Mwaka kilidaiwa kufungiwa kwa mmiliki
kujiita daktari badala ya tabibu!
Hata
hivyo wiki moja baada ya kuifungia kliniki hiyo kutoa huduma zake,
iliendelea kujitangaza kuwa inaendelea kufanya kazi kama kampuni ya
ushauri na huduma za kiafya na siyo kliniki tena.
Kutoka
jina la awali Fore Plan Clinic ilianza kujitangaza kama Fore Plan
Company kitendo ambacho Dk. Kingwangalla amekitaja kuwa ni kinyume na
sheria na kuagiza tabibu huyo akamatwe haraka iwezekanavyo.
No comments:
Post a Comment