KATIBU
Mkuu wa Baraza la Vijana wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Bavicha)
Julius Mwita amekamatwa na Jeshi la Polisi mchana huu katika Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam.
Mwita
na vijana wengine watatu ambao hawakufahamika majina yao mara moja
wamekamatwa kwa sababu ambazo hazijafahamika mpaka sasa wakati
wakisubiri Tundu Lissu Mwanasheria Mkuu wa Chadema kufikishwa mahakamani
hapo.
Mwandishi
ameshuhudia Mwita na vijana wawili wakikamatwa ndani ya eneo la
mahakama na kuingizwa ndani ya gari ya polisi yenye namba za usajili PT
1848.
Kijana
mwingine mmoja amekamatwa akiwa nje ya uzio wa mahakama hiyo ambapo
askari waliojihami kwa silaha za moto wameimarisha ulinzi ndani na nje
ya mahakama ya Kisut.
Vijana
wote wanne tayari wameondolewa mahakamni hapo na gari ya polisi ambapo
inaaminika kuwa watapelekwa Kituo Kikuu cha Polisi, Dar es salaam
kwaajili ya mahojiano.
No comments:
Post a Comment