Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. John Pombe Magufuli
anatarajiwa kuwa Mgeni rasmi siku ya Kilele cha maadhimisho ya siku ya
Vijana Kitaifa yatakayofanyika Mkoani Simiyu Oktoba 14 mwaka huu.
Kauli
hiyo imetolewa jana jijini Dar es salaam na Naibu Waziri Ofisi ya
Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Antony Mavunde
wakati wa mkutano na waandishi wa Habari.
Mhe
Mavunde alibainisha kuwa Kauli mbiu ya Siku ya Vijana mwaka huu ni
“Tokomeza umasikini kwa uzalishaji endelevu na matumizi yenye tija”.
Akifafanua
kuhusu kauli mbiu hiyo Mhe. Mavunde alisema lengo la kauli mbiu hii ni
kuzihimiza nchi wanachama wa umoja wa mataifa kushirikisha kikamilifu
Vijana katika shughuli za uzalishaji na kuhakikisha kuwa panakuwepo na
matumizi sahihi ya rasilimali za nchi kama vile ardhi,maji,madini na
Nishati ili kufikia shabaha ya kuwa na maendeleo endelevu ifikapo 2030.
Akizungumzia
maadhimisho hayo Kitaifa Mhe . Mavunde alisema kuwa vijana watapata
fursa ya kushiriki shughuli mbalimbali kama
makongamano,matamasha,michezo,maonnyesho ya Kazi za Vijana,Shughuli za
kujitolea na maandamano ya amani.
“Tanzania
tutasherekea siku ya Vijana Duniani Kitaifa kuanzia tarehe 8/10/2016 na
kilele kitakuwa tarehe 14/10/2016 Mkoani Simiyu ambapo Sherehe hii
itaenda sambamba na Maadhimisho ya kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa
Mwl. Julius Kambarage Nyerere, Wiki ya Vijana Kitaifa na kilele cha mbio
za Mwenge wa Uhuru mwaka 2016.” Alisisitiza Mhe. Mavunde.
Wazo
la kuwa na siku ya Vijana Duniani lilitolewa katika Mkutano wa Vijana
wa Kimataifa mwaka 1991 Mjini Vienna Australia kwa madhumuni ya kutafuta
njia ya kuchangisha fedha za kusaidia mifuko ya Taifa ya Vijana ambapo
mwaka 2000 nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa ikiwemo Tanzania zilianza
kuadhimisha siku ya Vijana Duniani kulingana na mazingira yake kwa
kuzingatia kauli mbiu ambayo huandaliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa
Mataifa.
No comments:
Post a Comment